OPERESHENI ya kuwaokoa watu waliopo ndani ya Feri iliyowaka moto kwenye Bahari ya Adriatiki zinaendelea. Watu 10 wamekufa katika ajali hiyo na wengine kadhaa wanahofiwa kupotea. Feri hiyo ilikuwa na abiria 478 pamoja na wafanyakazi huku Watu 41 hawajulikani walipo na maafisa wa Italia na Ugiriki wanajaribu kuthibitisha jumla ya watu waliokuwemo...
MABALOZI wa Mataifa ya Kiarabu wameidhinisha pendekezo la Palestina kuhusu marekebisho ya azimio la Umoja wa Mataifa la kutaka Israel kuacha kuikalia kwa mabavu Palestina katika kipindi cha miaka mitatu. Pendekezo hilo limepingwa na Israel pamoja na Marekani. Marekani imesisitiza kwamba lazima pawe na suluhisho la mazungumzo katika mzozo wa Israel na...
MWALIMU MKUU wa Shule ya Msingi ya Nyanguku iliyopo Halmashauri ya Mji wa Geita FRANCIS KATOTO amejeruhiwa baada ya kukatwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi. Tukio hilo limetokea usiku baada ya Majamzani hao kuvamia nyumba ya Mwalimu huyo na kupora...
WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO ametembelea Miradi ya umeme katika Vijiji mkoani Mara. Lengo la kutembelea Miradi hiyo ni kuhakikisha inakamilika mapema mwakani. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Profesa MUHONGO amesema Serikali imeamua kupeleka umeme Vijijini kwa lengo la kufuta Umasikini ikiwa ni pamoja na kuboresha Sekta ya Elimu kwa Shule za Sekondary za Kata ambazo ndio mkombozi kwa wananchi wengi wanaoishi...
Wakali kutoka Uganda Radio na Weasel huenda wakatiwa mbaroni mara baada ya kusabisha utata kwenye moja show waliyotakiwa kuifanya katika siku ya Boxing day huko Uganda lakini hawakutokea kwenye tamasha hilo hali iliyopelekea kuzuka kwa Ugomvi katika show hiyo amabapo baadae nguvu ya polisi ilihusika kutuliza mashabiki hao Kwa mujibu wa muandaaji wa show hiyo Radio na Weasel walilipwa kiasi cha shilingi milioni 9 za Uganda kama malipo ya awali Wasanii hao hawakuwepo nchini Uganda katika muda huo hivyo...
Klabu ya West Bromwhich Albion nimemfungashia virago kocha Alan Irvine ikiwa ni miezi saba tu toka apewe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kinachokipiga katika uwanja wa Hawthorns. Irvine raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 56 aliteuliwa kukinoa kikosi cha WBA baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Pepe Mel kutimuliwa, amekuwa akipata matokeo mabovu na kuwaacha klabu hiyo katika nafasi ya 16 ndani ya msimu wa ligi kuu nchini England. West Brom inataraji kusafiri kwenda jijini London kumenyana na...
Nahodha wa timu ya taifa ta Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji wa ulimwengu (Globe Soccer Award) huko nchini Dubai. Ronaldo amepata tuzo hiyo mbele ya wachezaji mbalimbali kama Messi, Neuer ambao ndio wapinzani wake wakubwa katika tuzo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani ballon d’Or inayotarajiwa kutolewa tarehe 12 januari 2015. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utoaji wa tuzo hizo, Ronaldo amesema anashukuru kwa kushinda tuzo hiyo na...
Hatimae Justin Bieber’s ametolewa kwenye club ya umoja wa mastar wanaomiliki ndege binafsi na hii imekuja mara baada ya Jb kugundulika kama ndege iliyokuwa inaaminika ni ya kwake hana umiliki nayo na ndege hiyo ipo sokoni kwa maaana inauzwa Bieber’s alipost picha instagram kuelekea siku ya Krismas akiwa kwenye ndege hiyo na kuandika caption ya maneno haya “New jet for Christmas, and she’s beautiful” Richa ya msanii huyo kutajwa kumiliki kiasi cha dola milioni 200 za kimarekani lakini ndege hiyo...
video ya wimbo mpya wa Nay wa mitego akadumba imeongozwa na Kevin Bosco Jnr ...
Wafanyakazi wa shughuli za uokozi wamefanikiwa kuwaokoa watu 265 kutoka ndani ya feri inayowaka moto ikiwa kwenye bahari kati ya Italia na Ugiriki na bado watu wengine 200 wamebaki ndani ya feri hiyo iitwayo Norman Atlantic. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Helikopta zimekuwa zikiwavuta watu kutoka feri hiyo iliyoshika moto Desember 28 mwaka huu...
Jukwaa la Katiba Tanzania-JUKATA limewataka wananchi kuisoma na kuielewa Katiba iliyopendekezwa huku wakilinganisha na Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 sanjari na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania HERBRON MWAKAGENDA amesema ili kufanikisha hilo Serikali inatakiwa iwezeshe upatikanaji wa nakala za kutosha za Katiba inayopendekezwa na Rasimu ya katiba ya Tume ya Mabadiliko...