WATU WAWILI wamefariki dunia akiwemo raia wa Kenya SUZAN BHOKE baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mpenzi wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya LAZARO MAMBOSASA amesema SUZAN amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito na anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la EDDY CLEMENT. Kamanda MAMBOSASA amebainisha chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na kwamba CLEMENT anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji...
RAIS JAKAYA KIKWETE leo anazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo Hatma kuhusu Sakata la Akaunti ya Tegeta ESCROW inasuburiwa kwa hamu. Sakata hilo limezusha mshikemshike Bungeni ambapo tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji FREDRICK WEREMA amejiuzulu kutokana na kutajwa moja kwa moja. Mawaziri Profesa SOSPETER MUHONGO Nishati na Madini,Profesa ANNA TIBAIJUKA Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini ELIAKIMU MASWI pia wanatakiwa kujiuzulu au Mamlaka za uteuzi kuwaondoa. Awali ilidaiwa...
Vinara wa Ligi kuu nchini England, klabu ya Chelsea leo wanashuka tena dimbani kumenyana na klabu ya Stoke City katika uwanja wa Brittania majira ya saa tano kamili usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki. Chelsea inayonolewa na kocha Jose Mourinho inaongoza ligi hiyo ikiwa na alama 39 sawa na klabu ya Manchester City iliyopata ushindi mnono wiki iliyopita dhidi ya Crystal Palace. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemuomba refarii wa mchezo huo wa leo, Swarbrick awe makini katika maamuzi...
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Australia Matthew Hayden ameshangazwa na maamuzi ya timu ya taifa ya England ya kumuacha nahodha wa zamani wa timu hiyo, Kevin Pietersen. Matthew amesema kitendo cha England kumuacha mmoja kati ya wachezaji hodari kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya nchi ya England kinaonyesha wazi hawapo teyari kwenda kushindana na timu kama India na Australia. England wametangaza majina ya wachezaji 15 watakaoshiriki michuano ya kombe la dunia huku ikimteua Eoin Morgan kuwa nahodha...
Mwanamke ambae hakutaka jina lake lifahamike ametuma barua pepe yenye kuelezea mahusiano yake na mkali kutoka Nigeria Wizkid ambapo ameeleza kuwa mahusiano yao ni ya muda mrefu na kuwa hivi karibuni alishea usiku mzito wa kimahaba na star huyo katika hoteli moja huko Lagos aliyoitaja kwa jina la Eko Binti huyo ametuma picha za baadhi ya vitu anavyomiliki star huyo ikiwemo tatoo iliyochorwa kwenye mwili wa Wizkid akiwa kitandani Binti huyo alienda mbali zaidi na kumtambia mpenzi wa Wizkid Tania...
KAMPUNI ya Kidoti inayojishughulisha na utengenezaji wa Nywele, Viatu, Mikoba na bidhaa mbalimbali leo imesaini mkataba wa dolla milioni tano kwa lengo la kujenga Ushirikiano na Kampuni ya Rainbow shell Craft ya Nchini China. Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kidoti, Jokate Mwegelo amesema ubia huo unalengo la kuiwezesha Kampuni ya Kidoti kuweza kupanua wigo wake kibiashara ikilenga pia kujiweka zaidi katika soko la Afrika Mashariki, Kati na Duniani. Amesema Kampuni hiyo ya China iliyowekeza nchini Tanzania...
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameidhinisha sheria mpya ya usalama ambayo inawezesha majasusi kunasa mawasiliano kisiri au kufanya udukuzi pamoja na kuwazuia washukiwa wa ugaidi kwa mwaka mmoja kabla ya kuwafungulia mashitaka. Kenyatta amesema kuwa sheria hiyo mpya inahitajika kwa ajili ya kukabiliana na tisho la ugaidi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab. Amesisitiza kuwa sheria hiyo haikiuki haki za binadamu wala kuwapokonya watu uhuru wa kujieleza. Hapo jana, wabunge wa serikali na wa upinzani walipigana...
MWILI wa aliyekuwa mnenguaji wa bendi za Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Mohamed Mbegu maarufu Aisha Madinda unazikwa leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yalitarajiwa kufanyika jana, lakini yalilazimika kuahirishwa baada ya Jeshi la polisi kuzuia hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi kutokana na utata wa kifo chake. Awali akizungumza na Efm, Mkurugenzi wa Asset, inayomiliki bendi ya Twanga pepeta, Asha Baraka amewataka watu wote kumwombea Marehemu Aisha ili mwenyezi mungu amlaze mahali pema...
WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amewataka wamiliki wote wa Viwanda nchini kutotupa ovyo taka zisizo tibiwa kwa dawa kwenye mito ya maji ili kupunguza athari zitokanazo na tatizo hilo kwa binadamu. Profesa Maghembe ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua rasmi ripoti ya utendaji wa Mamlaka za maji za Mikoa na miradi ya maji ya Kitaifa ya mwaka 2013-2014, kwa lengo la kuboresha huduma za maji nchini. Katika uzinduzi huo pia amesema kuwa hali ya upatikanaji...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, mwaka huu. Wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita. Awali kulikuwa na taarifa kuwa rais Kikwete angefanya mazungumzo hayo leo huku baadhi ya wadau na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii...
WAPIGANAJI wa Kikurdi wamesema wamepeleka kikosi Kaskazini mwa Iraq ili kupambana na wapiganaji wa kundi la Islamic State-IS. Kikosi cha Wakurd elfu nane 8, kimeanzisha Mashambulizi endelevu kuvunja zuio katika Mlima Sinjar ili kuwakomboa maelfu ya watu ambao wamezuiwa huko na Kundi la Islamic State. Operesheni hiyo imeanza Jumatano wiki hii kwa ushirikiano na vikosi vya Marekani na wafuasi wanaounga mkono harakati hizo....