Slider

MATAIFA TAJIRI NA MASKINI YABISHANA JUU YA NJIA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
Global News

MAZUNGUMZO ya Umoja wa Mataifa kuhusu ongezeko la joto duniani yanakamilika leo mjini Lima, Peru, huku mataifa tajiri na maskini ulimwenguni yakibishana kuhusu aina ya hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wanazostahili kuwasilisha katika mkutano wa kilele utakaoandaliwa mjini Paris Ufaransa, mwaka ujao. Katika ziara fupi aliyofanya kwenye mazungumzo hayo yanayoendelea kwa mjini Lima, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amezitaka serikali kumaliza kulumbana kuhusu ni nani anayestahili kufanya nini katika juhudi za...

Like
368
0
Friday, 12 December 2014
YAYA APATIKANA NA HATIA
Global News

MFANYAKAZI za Ndani wa Uganda ambaye alinaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amepatikana na hatia ya ukatili na hivyo atafikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu Disemba 15 mwaka huu. Jolly Tumuhirwe ameiambia Mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa. Hata hivyo waandishi wa habari wamezungumza na mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ambaye amekanusha madai ya Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja huku akihoji madai ya Jolly...

Like
353
0
Friday, 12 December 2014
MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA
Local News

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa –NEC, ya Chama Cha Mapinduzi –CCM, kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika  uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea na wanachama pamoja na wagombea wa nafasi za Uenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata za Ndoro...

Like
483
0
Friday, 12 December 2014
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI YAJENGA MAABARA 138
Local News

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kujenga maabara 138 ikiwa ni agizo la Rais JAKAYA KIKWETE la kutaka kila shule za Kata ziwe na Maabara. Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mhandisi MUSA NATTY wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri wakiwamo wasimamizi wa Maabara hizo. Mhandisi NATTY ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa wametimiza agizo la rais kwani awali walikuwa na maabara 12 na vyumba 126 hivyo kufanya idadi ya maabara...

Like
349
0
Friday, 12 December 2014
VIDEO: EFM YAWAASA VIJANA KUSHIRIKI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA
Local News

  Vijana wa  TANZANIA  wameaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki Chaguzi mbalimbali hususani huu wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desember 14 mwaka huu ili kupata viongozi bora kwa manufaa ya Taifa. Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa EFM Radio FRANCIS SIZA wakati wa mahojiano katika kipindi cha Joto la Asubuhi ambapo amesema kuwa ni wakati muafaka kwa vijana kutumia fursa hiyo kuchagua viongozi watakaosaidia nchi kufikia katika malengo ya kuwa na maendeleo pamoja na uchumi Imara. Amewaomba watanzania...

Like
315
0
Friday, 12 December 2014
40 WAFA KUTOKANA NA MLIPUKO WA MABOMU NIGERIA
Global News

MABOMU mawili yameripuka katika mji wa Jos nchini Nigeria, hilo likiwa ni shambulizi la pili kuukumba mji huo na kuwaua watu 40 huku wengine wakijeruhiwa. Taarifa zimeeleza kuwa hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na mashambulizi hayo lakini inashukiwa ni waasi wa kundi la Boko Haram wamefanya mashambulizi hayo. Mnamo mwezi Mei mwaka huu Boko Haram iliushambulia mji huo wa Jos ulioko kati mwa Nigeria na kuwaua watu 118.                                         ...

Like
506
0
Friday, 12 December 2014
CIA YATETEA MBINU ZAKE ZA KIKATILI KUWAHOJI WATUHUMIWA WA UGAIDI
Global News

MKURUGENZI wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, JOHN BRENNAN, kwa mara nyingine ametetea matumizi ya mbinu za kikatili wakati wa kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi baada ya shambulio la Septemba 11 nchini Marekani. BRENNAN amekiri kuwa baadhi ya mbinu zilizotumika zilikuwa za kuchukiza. Lakini amesisitiza kuwa baadhi ya wafungwa ambao walipitia mbinu hizo, ambazo zilikuwa ni pamoja na kuwazamisha kwenye maji, kuwafadhaisha na kuwanyima usingizi zimesaidia kuokoa maisha ya Wamarekani na zilisaidia kumpata OSAMA BIN LADEN. Amejibu ripoti ya Kamati...

Like
327
0
Friday, 12 December 2014
RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA TAASISI TOFAUTI SERIKALI NA MAHAKAMA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa -PDB. Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa...

Like
285
0
Friday, 12 December 2014
LOWASSA: SERIKALI YA KIKWETE IMEFANYA MAKUBWA
Local News

MBUNGE WA MONDULI na waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa EDWARD LOWASSA amesema Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais JAKAYA KIKWETE imefanya makubwa ikiwa ni pamoja na usambazaji Umeme na Maji Vijijini. Mheshimiwa LOWASSA ameeleza hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Viongoji huko Bwawani Mto wa Mbu Wilayani Monduli. Amebainisha kuwa haijawahi kutokea Serikali ya Rais KIKWETE imefanya makubwa katika Umeme, Barabara na Maji na kwamba wakati akiwa Waziri wa Maji...

Like
316
0
Friday, 12 December 2014
WHO: IDADI YA WALIOKUFA KWA EBOLA YAONGEZEKA, CHANJO YALETA MATUMAINI
Global News

SHIRIKA la afya la Kimataifa WHO, limesema idadi ya waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola imeongezeka na kufikia watu 5689. Jumla ya watu 16, 000 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo  katika nchi nne-shirika hilo la Umoja wa mataifa linasema. Mataifa matatu ya Afrika Magharibi, Guinea, Sierra Leone na Liberia ndio yaliyoathirika zaidi na maradhi hayo. Katika hatua nyingine Watafiti wa chanjo ya Ebola nchini Marekani wamesema kuwa wametiwa moyo na matokeo ya awamu ya kwanza ya majaribio ya chanjo ya ugonjwa...

Like
384
0
Thursday, 27 November 2014
MISIKITI ILIYOFUNGWA YAFUNGULIWA MOMBASA
Global News

MISIKITI  minne iliofungwa na maafisa wa polisi wiki iliopita baada ya kuchukuliwa na vijana wenye itikadi kali za kiislamu hatimaye imefunguliwa. Hatua ya kuifungua misikiti hiyo ya Minaa, Sakina, Musa na Swafaa inajiri baada ya siku mbili za mazungumzo kati ya viongozi wakuu wa kiislamu, wataalam na uongozi wa kaunti ya Mombasa. Maelezo ya mazungumzo hayo yalioandaliwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na kaunti kamishna Nelson Marwa yamefanywa kuwa siri. Kabla ya misikiti hiyo kufunguliwa ,viongozi wa kiislamu pamoja...

Like
281
0
Thursday, 27 November 2014