Slider

MHUBIRI WA CANADA APIGWA KIFUNGO CHA MAISHA KOREA KASKAZINI
Global News

MAHAKAMA ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu. Hyeon Soo Lim, mwenye umri wa maika 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.” Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la...

Like
329
0
Wednesday, 16 December 2015
MAFURIKO: WAZIRI  JENISTA MHAGAMA AFANYA ZIARA BOKO BASIHAYA
Local News

KUFUATIA eneo la boko Basihaya  kuwa na tatizo la kujaa maji kwa wingi pindi mvua inapo nyesha  hali inayo pelekea mafuriko, Waziri ofisi ya waziri mkuu sera ,bunge vijana ,ajira na walemavu mheshimiwa JENISTA MHAGAMA leo amefanya ziara katika eneo hilo  ili kujionea hali ilivyo  . Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo yalio athiriwa na maji mheshimiwa Waziri amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni pamoja na watendaji wake kuhakikisha wanaripoti Wizarani leo saa kumi jioni wakiwa na maelezo ya...

Like
494
0
Wednesday, 16 December 2015
WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAMETAKIWA KUSIMAMIA MIKAKATI YA KUDHIBITI KIPINDUPINDU
Local News

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto  na Wazee imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie utekelezaji wa mikakati yote ya kudhibiti mlipuko wa kipindupindu ikiwa  ni pamoja na kusimamia kanuni za afya na kuhakikisha kuwa wanadhibiti ugonjwa huo  kwa kutoa taarifa ya utekelezaji kila siku .   Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam  Waziri wa Wizara hiyo  Mheshimiwa  Ummy Mwalimu amesema licha ya kasi ya ongezeko la ugonjwa huo kupungua Dar es salaam kutoka wastani wa...

Like
259
0
Wednesday, 16 December 2015
DONALD TRUMP AKOSOLEWA VIKALI
Global News

WAGOMBEA wa Republican wanaowania nafasi ya urais nchini Marekani wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea kwa mashambulio ya California na Paris. Mgawanyiko mkubwa umetokea kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea haki za kiraia. Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani, huku Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, akimwita Trump...

Like
252
0
Wednesday, 16 December 2015
MIILI YA WATU 19 YAPATIKANA MEXICO
Global News

MIILI ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana. Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco. Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo....

Like
215
0
Wednesday, 16 December 2015
WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA WAMETAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA
Local News

SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa.   Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.   Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kila mtumishi wa umma anapaswa...

Like
198
0
Wednesday, 16 December 2015
MAWAKILI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YA SHERIA
Local News

JAJI MKUU wa Tanzania Mheshimiwa Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama.   Akizungumza na Mawakili wapya 104 waliohitimu Shule ya Sheria  kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, amesema kuwa...

Like
233
0
Wednesday, 16 December 2015
UJERUMANI YAPUUZA WITO WA MAREKANI
Local News

WAZIRI wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von Der Leyen amepuuza wito wa Marekani wa kuitaka Ujerumani kuchangia zaidi kijeshi katika kukabiliana na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS. Von Der Leyen amesema Ujerumani tayari inapambana dhidi ya makundi yenye itikadi kali ikiemo nchini Mali na Afghanistan na kuongeza kuwa Ujerumani inatuma ndege za kufanya shughuli za upelelezi nchini Syria zinazohitajika kwa dharura. Hata hivyo Waziri huyo wa Ulinzi wa Ujerumani amesema ataiandikia Marekani kuifahamisha kuwa...

Like
222
0
Tuesday, 15 December 2015
MATAIFA 34 YA KIISLAM KUUNGANA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI
Global News

SAUDI ARABIA imetangaza kuunda muungano mpya wa kijeshi wa nchi 34 za kiislamu kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ugaidi. Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo cha pamoja mjini Riyadh. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kuwa muungano huo utaratibu juhudi za mapigano dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri na...

Like
194
0
Tuesday, 15 December 2015
WAHITIMU WA UWAKILI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA KAZI ZA MAHAKAMA
Local News

WAHITIMU wa taaluma ya Uwakili Nchini wametakiwa kuzingatia sheria na kufuata utaratibu katika kufanya kazi za mahakama ili kusaidia haki kutendeka katika jamii. Wito huo umetolewa leo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George  Masaju alipozungumza katika hafla ya kuapishwa kwa Mawakili wapya zaidi ya 100 jijini Dar es salaam na kusema kuwa kitendo cha Wakili kufanya kazi bila kufuata kanuni na utaratibu wa kazi hiyo ni kosa na hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi yao. Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania...

Like
259
0
Tuesday, 15 December 2015
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AANZA KAZI RASMI
Local News

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, dokta Hussein Mwinyi, aliyeteuliwa na kisha kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu ameripoti ofisini na kuanza kazi rasmi.   Waziri Mwinyi amewasili ofisini kwake na kulakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Majeshi Mnadhimu Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, wanajeshi na watumishi wa Umma wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Job Masima.   Akizungumza na Menejimenti ya Wizara, Waziri Mwinyi amesema matarajio...

Like
225
0
Tuesday, 15 December 2015