Slider

KANYE WEST ALAZWA HOSPITALI LOSS ANGELES
Slider

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Kanye West amelazwa hospitalini mjini Los Angeles, vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti. Msemaji wa polisi ameambia BBC kwamba walipokea simu ya kutokea kwa mtafaruku Jumatatu adhuhuri, lakini hawakutaja jina la mwanamuziki huyo. Baadaye, mtafaruku huo ulidaiwa kuwa tukio la kimatibabu, na maafisa wa kutoa huduma ya dharura walifika eneo hilo. Msemaji wa maafisa wa huduma za dharura wa LA amesema mwanamume ambaye jina lake halikutajwa alipelekwa hospitalini “kufanyiwa uchunguzi zaidi”....

Like
530
0
Tuesday, 22 November 2016
RAIA WA NIGERIA ALIYEKUTWA NA BANGI KUNYONGWA SINGAPORE
Slider

Singapore imekataa ombi la msamaha kutoka kwa raia mmoja wa Nigeria ambaye amepangiwa kunyongwa Ijumaa kwa kupatikana na bangi, shirika la haki za kibinadamu la Amnesty International limesema. Familia ya Chijoke Stephen Obioha ilifahamishwa kuhusu hatua hiyo Jumatano. Obioha alipatikana na kilo 2.6 za bangi Aprili 2007, kiasi kilichokuwa kimezidi kipimo cha gramu 500 ambacho mara moja humfanya mtu kuhukumiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya chini ya sheria za Singapore. Afisa wa Amnesty International Rafendi Djamin amesema shirika hilo...

Like
290
0
Thursday, 17 November 2016
MKWASA ALIA NA WACHEZAJI
Slider

Dar es Salaam. Siku moja baada ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa amesema ni vigumu kupima viwango vya wachezaji hasa wa Tanzania. Ligi hiyo imemaliza mzunguko wa kwanza huku baadhi ya wachezaji waliong’ara msimu uliopita wakishindwa kufanya hivyo msimu huu huku wachezaji wengine wakiibuka na kung’ara. Baadhi ya wachezaji waliong’ara raundi ya kwanza ni Shiza Kichuya, Omar Mponda, Simon Msuva wameng’ara raundi ya kwanza...

Like
228
0
Monday, 14 November 2016
TRUMP KUWAREJESHA WAHAMIAJI KWAO
Slider

Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo. Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake . Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama. Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka...

Like
257
0
Monday, 14 November 2016
DONALD TRUMP AFANYA UTEUZI WA AWALI
Slider

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi. Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo. Stephen Bannon, alikuwa ni...

Like
214
0
Monday, 14 November 2016
NOTI ZA RUPEE 500 NA 1000 KUFUTWA INDIA
Slider

Waziri mkuu wa India Narendra Modi ametangaza kuwa noti ya Rupee 500 na ile ya 1000 zitaondelewa katika mfumo wa fedha kwa siku moja. Hatua hiyo ya kushangaza ni mijawapo ya harakati za kukabiliana na Ufisadi pamoja na ukopeshaji wa fedha wa haramu alisema katika runinga. Benki zitafungwa siku ya jumatano huku huduma za mashine za kutoa pesa za ATM zkisitishwa. Noti mpya za rupee 500 na 2000 zitawekwa katika mfumo wa fedha ili kuchukua mahala pake noti hizo zilizoondolewa....

Like
300
0
Wednesday, 09 November 2016
SAMSUNG KWENYE TUHUMA ZA UFISADI WA KISIASA
Slider

Waendesha mashtaka nchini Korea kusini wamevamia ofisi za kampuni ya kielektoniki ya Samsung kama sehemu ya uchunguzi wa sakata ya kisiasa inayomuhusu rais Park Geun-hye. Waendesha mashtaka wanachunguza madai kwamba Samsung ilimpatia pesa mtoto wa kike wa Choi Soon-sil, ambaye ni rafiki wa karibu wa rais. Bi Choi anashutumiwa kutumia urafiki wao kuingilia kati siasa na utoaji wa zabuni za kibiashara. Samsung imeithibitishia BBC kuwa uvamizi huo ulifanyika ikisema “hakuna maelezo zaidi “. Rais Park ameomba msamaha kwa uhusiano wa...

Like
300
0
Tuesday, 08 November 2016
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SPIKA WA BUNGE KUFUATIA KIFO CHA SPIKA MSTAAFU, SAMWEL SITTA
Slider

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora Samwel Sitta. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujeruman alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita. Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa hizo na kwamba Taifa limempoteza...

Like
494
0
Monday, 07 November 2016
MADINI MAPYA YAGUNDULIWA MERERANI, TANZANIA
Slider

Madini mapya yamegunduliwa nchini Tanzania, katika eneo lenye madini ya kipekee la Manyara, na kupewa jina Merelaniite. Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika milima ya Lelatema katika wilaya ya Simanjiro katika eneo la Manyara. Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya Tanzanite. Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia...

Like
406
0
Wednesday, 02 November 2016
MGOMO WAPELEKEA CHUO CHA MAKERERE KUFUNGWA
Slider

Wanafunzi wameanza kuondoka kutoka Chuo Kikuu cha Makerere baada ya Rais Yoweri Museveni kutangaza kifungwe mara moja Jumanne jioni. Rais alisema amechukua hatua hiyo “kuhakikisha usalama wa watu na mali.” Chuo kikuu hicho kilikuwa kimekumbwa na vurugu kutokana na mgomo wa wahadhiri na wanafunzi. Chama cha wahadhiri Jumatatu kiliamua kuendelea na mgomo hadi wahadhiri walipwe marupurupu ya miezi minane ambayo yamefikia Sh32bn (dola 9.2 milioni za Marekani). Wanafunzi walijiunga na mgomo Jumanne, na walitaka kukutana na Rais Museveni...

Like
365
0
Wednesday, 02 November 2016
MFALME MTEULE WA THAILAND KUTHIBITISHWA DECEMBER
Slider

imetaarifiwa kwamba mfalme mteule mtarajiwa wa Thailand Vajiralongkorn atathibitishwa rasmi kama mfalme ajaye mnamo Desemba mosi. Mwana wa mfalme huyo ambaye pia ni mfalme mtarajiwa alitarajiwa kupakwa mafuta na kutawazwa katika kipindi ama baada ya maziko ya babake , mfalme King Bhumibol Adulyadej, aliyefariki wiki tatu zilizopita, kutokana na yeye mwenyewe kuomba muda wa kumuomboleza babake. Mpaka sasa haijafahamika wazi, ni uhusiano wa namna gani mfalme huyo mtarajiwa atakuwa nao baina yake na vikosi vya jeshi la serikali ambavyo hivi...

Like
278
0
Wednesday, 02 November 2016