MIAKA miwili tangu machafuko yalipoanza Sudan kusini, mashirika ya misaada yametahadharisha kuhusu upungufu mkubwa wa chakula unaotarajia kuikumba nchi hiyo na kutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kumaliza vitendo vya uhalifu wa kivita ndani ya Taifa hilo. Ingawa makubaliano ya amani yalitiwa saini miezi kadhaa iliyopita, machafuko bado yanaendelea na karibu watu milioni moja na laki Tano wamelazimika kuyahama makazi yao. Tangu kuanza kwa mapigano nchi nzima miaka miwili iliyopita, Rais na makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo...
WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry yupo nchini Moscow kwa ajili ya mazungumzo na Rais Vladimir Putin kuhusu njia za kumaliza vita vinavyoendelea nchini Syria. Mazungumzo hayo yanalenga kupunguza mfarakano kati ya Urusi na Marekani, hasa kuhusu makundi ambayo yanafaa kujumuishwa kwenye mazungumzo ya mzozo huo. Urusi ambayo inamuunga mkono Rais wa Syria Bashar Al-Assad, imesema mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wa makundi yanayopinga serikali ya Syria haukuwakilisha makundi yote yanayovutana katika mzozo...
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya umesema hautawavumilia watumishi wa hospitali ya Mkoa wa Kagera wanaojihusisha na vitendo vya kughushi nyaraka za kuchukulia dawa katika maduka ya dawa na kuusababishia Mfuko kulipa fedha ambazo hazijatumika kihalali. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Michael Mhando ameyasema hayo mkoani humo wakati akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera kabla ya uzinduzi wa mpango wa Madaktari Bingwa ili kusaidia kutoa huduma kwa wanachama na wananchi kwa ujumla. Mhando...
WIZARA ya Nishati na Madini imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi One na Two unakamilika ifikapo mwezi Februari mwaka 2016 na kuanza uzalishaji ili kuongeza kiasi cha nishati ya umeme kufikia zaidi ya Megawati 100. Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini dokta Medadi Kalemani alipofanya ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam....
KUNDI kuu la kiislamu nchini Nigeria linaloungwa mkono na waislamu wa Kishia wa Iran, linasema kuwa mke wa kiongozi mkuu Sheikh Ibrahim Zakzaky, ameuwawa katika makabiliano na jeshi kaskazini mwa mji wa Zaria. Vuguvugu la kiislamu nchini Nigeria (IMN) linadai kuwa Zeenat Ibraheem ameuwawa kwa pamoja na mwanaye Sayyid Ibraheem Zakzaky. Sheikh Zakzaky alikamatwa na wanajeshi waliozingira nyumba yao kufuatia madai kuwa wanachama wa kundi hilo walijaribu kumuua kamanda mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai huko Zaria siku...
MAAFISA wa upelelezi wa ajali za ndege kutoka Misri wamesema kuwa hawajapata ushahidi wowote kuwa ndege ya Urusi iliyoanguka katika rasi ya Sinai na kuua watu 224 ililipuliwa. Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Sharm el-Sheikh ikielekea Moscow ilianguka jangwani mwezi Oktoba. Kundi moja la wapiganaji wanaoliunga mkono kundi la Islamic State –IS, walidai kuwa wao ndio walioidungua ndege...
IMEELEZWA kuwa Jimbo la Mbagala linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira kwa vijana pamoja na elimu ya ujasiliamali . Mbunge wa Mbagala Issa Ali Mangungu kupitia chama cha mapinduzi -ccm- ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya kituo cha elimu na mafunzo ya afya –KEWOVAC- Amesema kuwa wilaya nzima ya Temeke kuna chuo kimoja tu cha ufundi hali inayosababisha vijana wengi kushindwa kupata ujuzi ambao utawakwamua kiuchumi na badala yake huishia...
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameahidi kushirikiana na Waandishi wa habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari ili kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya habari Nchini. Waziri Nape ameyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari pamoja na Wafanyakazi wa Wizara hiyo alipoingia Wizarani hapo kuanza kazi rasmi ambapo amesema amekusudia kuwa mlezi wa wanahabari pamoja na vyombo vya habari huku akimtaka kila mtu katika tasnia hiyo kutekeleza wajibu wake kwa kufuata misingi...
Wakati Chelsea kukipiga tena na Paris St-Germain, Ratiba ya hatua ya 16 bora michuano ya klabu bingwa barani Ulaya HII NDIO RATIBA KAMILI Gent v Wolfsburg Roma v Real Madrid Paris St-Germain v Chelsea Arsenal v Barcelona Juventus v Bayern Munich PSV Eindhoven v Atletico Madrid Benfica v Zenit St Petersburg Dynamo Kiev v Manchester City...
SERIKALI ya Marekani imeshauri Raia wake walio nchini Burundi kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo baada ya watu 87 kuuawa kwenye ghasia zilizotokea siku ya Ijumaa. Ghasia zilizojitokeza kwenye mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura ni mbaya zaidi tangu kuanza kwa vurugu mwezi Aprili mwaka huu , baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania tena urais kwa muhula wa tatu. Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo ya...
MAHAKAMA ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikishughulikia kesi za mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita leo itatoa hukumu yake ya mwisho kabla ya kufungwa rasmi. Hukumu hiyo itakuwa dhidi ya watuhumiwa Pauline Nyiramasu ambaye ni waziri wa zamani wa Maendeleo ya wanawake nchini Rwanda na mtoto wake ambaye wote wamekana mashtaka yanayowakabili. Mahakama hiyo ambayo imekuwa nchini katika mji wa Arusha ilikuwa ikisikiliza kesi za watuhumiwa wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka...