IMEELEZWA kuwa watu wenye ulemavu wanakabilwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za kijamii. Hayo yamebainishwa hii leo katika maadhimisho ya watu wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya furahisha jijini mwanza. Akisoma risala kwa niaba ya watu wenye ulemavu Blandina Sembo amesema huduma za kijamii zimekuwa miongoni mwa changamoto kubwa kwa walemavu hasa wa kundi la wasiosikia kwa kukosa taarifa muhimu za...
MTU mmoja raia wa Uingereza, anayetuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi, amefungwa jela miaka tisa na mahakama mjini Mombasa nchini Kenya. Jermaine Grant Mwingereza aliyekamatwa mwaka 2011, amefungwa jela kwa makosa tisa yanayohusiana na kujaribu kujipatia uraia wa Kenya kwa njia haramu. Bado anakabiliwa na mashtaka ya “kupanga kuunda vilipuzi” kwenye kesi ambayo bado inaendelea mjini Mombasa lakini Grant amekanusha mashtaka hayo....
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haina mpango wa kufunga maduka ya dawa baridi yaliyopo katika maeneo ya Hospitali za Serikali ispokuwa mpango waliokuwa nao ni kuhakikisha kuwa wanaimarisha upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu pamoja na kuboresha huduma muhimu ziweze kupatikana kwa ubora na haraka zaidi. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Donan Mmbando wakati wa ziara yake ya Hospitali ya Taifa ya...
KATIBU MKUU Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi. Balozi Sefue ametoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine. Amesema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina...
HATIMAYE Makontena tisa yalio kamatwa jana maeneo ya mbezi tangi bovu mali ya kampuni ya HERITAGE EMPIRE COMPANY LIMITED yamefunguliwa na kukaguliwa na kukutwa na malighafi za ujenzi wa kiwanda. Makontena hayo tisa ambayo yana milikiwa na kampuni ya HERITAGE EMPIRE yameanza kukaguliwa toka jana jioni na kukamilika leo ambapo e fm imeshuhudia ukaguzi huo na kukuta malighafi mbalimbali za ujenzi kama vile vyuma vikubwa vyenye uwezo wa kujenga kiwanda cha ukubwa wa square mita za mraba elfu nne vitu...
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterenia imepungua kwa mara ya kwanza mwezi wa Novemba ikilinganishwa na mwezi mmoja kabla. Inakadiriwa kuwa wakimbizi laki moja na elfu 40 wameingia Ulaya mwezi uliopita wakipitia baharini. Habari hizo zimetangazwa na shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR mjini geneva jana....
WAFANYIBIASHARA wakubwa wametajwa kuwa ni miongoni mwa watu mafisadi zaidi sawa na maafisa wa polisi Barani Afrika. Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa na shirika la kuchunguza ufisadi duniani “Transparency International”. Ni mara ya kwanza kwa wafanyabiashara kutajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani na Shirika hilo limeongeza kwamba matumizi mabaya ya mamlaka yanasababisha ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji...
UONGOZI wa Muungano wa Wafanyabiashara wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam MUMADA waliopo Soko la Kibasila wameilalamikia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushindwa kurekibisha uchakavu wa miundombinu ya majitaka, mazingira pamoja na majengo ya soko hilo la Kibasila licha ya Manispaa hiyo kukusanya ushuru wa kutosha kuboresha hali ya mazingira katika soko hilo. Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Muungano wa Wafanyabiashara Masoko kanda ya Ilala Issa Malisa amesema uongozi hauko tayari kuona kampuni...
SERIKALI imesema imeanza uchunguzi wa ufisadi wa Dola milioni 6 uliohusu mkataba wa mkopo kati ya benki ya Stanbic na serikali. Jumatatu, mahakama nchini Uingereza iliamuru kulipwa kwa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania baada ya taasisi ya uchunguzi wa makosa makubwa ya ufisadi ya Uingereza kuwasilisha ushahidi kwamba kiasi hicho cha fedha kilipotea wakati wa uuzwaji wa hati fungani za Serikali kwa benki ya Stanbic Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema ni uchunguzi wa benki kuu ya Tanzania...
RAIS wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa ahadi zinazotolewa na viongozi zinahitaji kutekelezwa ili kuuokoa ulimwengu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Hollande ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dunia mjini Paris kwa lengo la kujadili juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Katika mkutano huo Viongozi hao wameahidi kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ya mkaa inayosababisha viwango hivyo vya joto...
ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Burkina Faso ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu wa Zamani wa nchi hiyo Uroch Christian Kabore ameshinda kwa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku chache zilizopita. Waziri Mkuu huyo wa zamani amepata alisimia 53.5 katika Uchaguzi huo unaoaminika kuwa ni wa kwanza tangu maandamano yaliyomuondoa madarakani Rais wa miaka mingi Blaise Compaore. Uchaguzi Mkuu ulitarajiwa kufanyika mwezi uliopita lakini ukacheleweshwa na jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu mwezi Septemba mwaka...