Slider

NDEGE ILIYOANGUKA MISRI ILILIPULIWA
Global News

NCHI ya Urusi imethibitisha kuwa ajali ya ndege ya Metrojet iliyoanguka na kuua watu zaidi ya 200 katika rasi ya Sinai nchini Misri mwezi uliopita iliangushwa na shambulio la kigaidi. Mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Alexander Bortnikov amemueleza rais wa nchi hiyo Vladimir Putin kuwa ndege hiyo iliangushwa na bomu lenye uzani wa kilo moja. Bortnikov alipokamilisha maelezo yake kwa rais Putin, rais huyo pamoja na mawaziri wengine wakuu wamesimama na kunyamaza kimya kwa muda kabla ya rais Putin...

Like
209
0
Tuesday, 17 November 2015
BOMOABOMOA KUANZA KINONDONI
Local News

MANISPAA ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.   Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayosababisha Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hilo la ubomoaji kwa kuhusisha nyumba zote zilizojengwa Bila kibali cha ujenzi na Bila kufuata michoro ya mipango miji   Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi yaliyokusudiwa na...

Like
339
0
Tuesday, 17 November 2015
JOBU NDUGAI ATANGAZWA KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11
Local News

ALIYEKUWA Mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jobu Ndugai amefanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kushinda katika Uchaguzi uliofanyika leo Bungeni mjini Dodoma.   Mwenyekiti wa Muda wa kikao cha kumpata Spika, mheshimiwa Andrew Chenge amesema Mheshimiwa Ndugai ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 254 sawa na Asilimia 70 kati ya kura 365 zilizopigwa na wabunge wote wa Bunge hilo. Kwa upande wake Spika wa bunge hilo Mheshimiwa Jobu Ndugai amewashukuru...

Like
288
0
Tuesday, 17 November 2015
ANDY MURRAY AANZA VYEMA MICHUANO YA TENNIS
Global News

Muingereza Andy Murray anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani ameanza vema michuano ya dunia ya tenesi kwa ushindi. Murray alimshinda mpinzani wake David Ferrer, wa Hispania, ambae anashikia nafasi ya saba kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa jumla ya seti 6-4 6-4. Nae Rafael Nadal, akamchapa Stan Wawrinka kwa jumla ya seti 6-3 na 6-2, hivyo Nadal kulipa kisasi cha kufungwa na Wawrinka katika michuano ya Paris Masters, mchezo huu ulitumia muda wa saa moja na dakika 23....

Like
214
0
Tuesday, 17 November 2015
UFARANSA YATANGAZA VITA DHIDI IS
Global News

RAIS Francoise Hollande wa Ufaransa ametangaza kwamba nchi yake ipo kwenye vita dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu( IS).   Akihutubia mabaraza mawili ya bunge jana, Rais Hollande ameapa kuwa nchi yake ipo tayari kuliangamiza kundi hilo linaloendelea kuleta madhara makubwa katika nchi mbalimbali.   Kiongozi huyo amesema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa atahakikisha vikosi vya ulinzi vinaimarishwa na kutaundwa muungano wa kimataifa kwaajili ya kudhibiti mipaka....

Like
202
0
Tuesday, 17 November 2015
GUINEA: MGONJWA WA MWISHO WA EBOLA APONA NA KURUHUSIWA
Global News

MAAFISA wa Afya nchini Guinea wamesema mgonjwa wa mwisho aliyeripotiwa kupata maradhi ya Ebola amepona na ameruhusiwa kutoka kwenye kituo cha matibabu kilichopo mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry. Ugonjwa huo ulioanza nchini Guinea, umeua zaidi ya watu 11,000 Afrika magharibi ingawa tayari Nchi jirani za Sierra Leone na Liberia zimefanikiwa kuutokomeza ugonjwa huo. Mgonjwa mmoja aliyekuwa amebaki ni mtoto wa siku 19 ambaye mama yake alifariki kutokana na ugonjwa huo huku msemaji wa kitengo kinachoratibu mapambano dhidi ya Ebola...

Like
262
0
Tuesday, 17 November 2015
UTAFITI: KATI YA WATOTO 200 ASILIMIA SITA WANAVUTA TUMBAKU
Local News

UTAFITI uliofanywa na Chama cha Afya ya jamii (TPHA) unaonesha kwamba kati ya watoto 200 Asilimia sita ya watoto hao wanajihusisha na uvutaji wa Tumbaku. Akazingumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mratibu kutoka chama cha Afya  ya jamii (TPHA), BERTHA MAEGA amesema kuwa utafiti huo umehusisha watoto wa shule ya msingi kuanzia darasa la nne hadi la sita huku wengi wao wakikiri kushawishiwa na wazazi na marafiki. BERTHA amesema kuwa ili kuweza kudhibiti tatizo hilo kuna umuhimu...

Like
307
0
Tuesday, 17 November 2015
BUNGE LA 11 LAANZA MCHAKATO WA KUMPATA SPIKA
Local News

BUNGE la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeanza kikao chake cha kwanza kwa mchakato wa kumpata Spika wa Bunge hilo atakayeongoza kwa muda wa miaka mitano. Miongoni mwa wagombea wanaowania Nafasi ya Uspika ni pamoja na Jobu Ndugai kutoka-CCM, Goodluck Ole Medeye wa CHADEMA, Peter Sarungi wa AFP, Hassan Almas kutoka NRA na Godfrey Malissa wa chama cha CCK. Hata hivyo Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

Like
443
0
Tuesday, 17 November 2015
BAN KI-MOON KUANZA ZIARA KOREA KASKAZINI
Global News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anatarajiwa kufanya ziara nchini Korea Kaskazini, na hivyo kuwa kiongozi wa kwanza wa umoja huo duniani kuizuru nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita.   Shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap, limesema kuwa Ban atazuru Korea Kaskazini baadae wiki hii, ingawa tarehe kamili bado haijatangazwa.   Hata hivyo taarifa kutoka ngazi za juu za Umoja wa Mataifa zimeeleza kwamba Ban alikuwa tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un,...

Like
228
0
Monday, 16 November 2015
UGANDA NA KENYA ZAIMARISHA USALAMA
Global News

NCHI za Uganda na Kenya zimeimarisha usalama kufuatia mashambulio yaliyojitokeza mjini Paris mwishoni mwa wiki lengo ikiwa ni  kuzuia mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu. Msemaji wa polisi nchini Uganda amesema polisi na wanajeshi wameimarisha doria kuzuia mashambulio, hasa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab kutoka Somalia. Nchini Kenya, usalama pia umeimarishwa mipakani na katika miji mikuu, na kuwataka wananchi kutoa taarifa haraka mara wanapoona kitu au mtu yeyote wanayemtilia...

Like
202
0
Monday, 16 November 2015
CCM YAMPITISHA JOB NDUGAI KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE
Local News

KAMATI ya Wabunge wote wa chama cha Mapinduzi-CCM-imempitisha Ndugu Job Ndugai kuwa mgombea wa Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia wagombea wenzake wa chama hicho kujitoa katika kinyang’anyiro hicho.   Akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa mgombea huyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa-CCM-Nape Nnauye amesema wana imani na Ndugai kuwa atashinda katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake wa kuongoza.   Kabla ya Ndugai kutangazwa kuwa ndiye atakayewania Uspika, wengine waliokuwepo katika kinyang’anyiro hicho ni...

Like
191
0
Monday, 16 November 2015