Slider

RAIS MAGUFULI APOKEA SALAMU ZA PONGEZI KUTOKA KWA MALKIA ELIZABETH II
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Katika salamu hizo Malkia Elizabeth amemueleza Rais dokta Magufuli kuwa  anatumaini mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea kuwa mazuri wakati wa utawala wake.   Katika hatua nyingine Mfalme Akihito wa Japan amemueleza Mheshimiwa Magufuli nchi yake ipo...

Like
256
0
Monday, 16 November 2015
UFARANSA YAFANYA MASHUMBULIZI DHIDI YA IS
Global News

UFARANSA imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya kundi la Dola la Kiislamu katika mji wa Raqqa, nchini Syria. Mashambulizi hayo ya anga ni ya kwanza kufanywa na Ufaransa tangu mji wake mkuu, Paris, kushambuliwa usiku wa Ijumaa na kundi hilo, ambapo watu 132 waliuawa. Maafisa wa Ufaransa wamesema mabomu 20 yaliangushwa na ndege zaidi ya kumi, zilizoruka kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu na Jordan, kwa kushirikiana na kituo cha kijeshi cha...

Like
179
0
Monday, 16 November 2015
SHAMBULIO LEBANON: TISA WAKAMATWA
Global News

IDARA za Usalama nchini Lebanon zimefanikiwa kuwakamata watu Tisa wanaodhaniwa kuhusika katika shambulio lililotokea Alhamisi ya wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Taarifa zinaeleza kwamba watu Saba kati ya tisa wanaoshikiliwa na Polisi ni raia wa Syria huku wengine wawili ni raia wa Lebanon huku tayari kundi la wapiganaji wa Kiislamu limedai kuhusika na shambulio hilo. Hata hivyo Wachunguzi wamebaini kuwa washambuliaji hao waliilenga hospitali inayoendeshwa na taasisi ya wapiganaji wa majeshi ya Kilebanon ya madhehebu...

Like
191
0
Monday, 16 November 2015
JAMII YA WAFUGAJI IMETAKIWA KUTOKOMEZA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Local News

JAMII ya wafugaji imetakiwa kutumia juhudi katika kubadili mitazamo ya watu juu ya matumizi ya mila na desturi ili kusaidia kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kuleta maendeleo kwa Taifa.   Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii Bi. Rose Haji Mwalimu wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la viongozi wa mila wa kabila la wamasai na wanawake Mashuhuri lenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo.   Bi. Rose amewataka...

Like
241
0
Monday, 16 November 2015
CHIEF YEMBA ATANGAZA KUWANIA KITI CHA USPIKA WA BUNGE
Local News

ALIYEKUWA mgombea urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Chief Lutayosa Yemba, ametangaza kugombea kiti cha Uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.   Chief Yemba, ameyasema hayo jijini Arusha, alipokuwa akitoa Tathimini yake kwa vyombo vya habari kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu, pamoja na tathimini ya uchaguzi wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu.   Amesema baada ya kuanguka...

Like
460
0
Monday, 16 November 2015
EFM VS KAWE VETERANI 3-3
Local News

Dakika 90 za mchezo wa kirafiki kati ya E-fm Vs Kawe Veterani zilimalizika kwa sare ya magoli 3-3, huku E-fm wakiwa wa kwanza kuliona lango la Kawe Veterani katika kipindi cha kwanza cha mchezo. Mchezo huo wa kusisimua ulishuhudiwa na wakazi wa Kawe katika uwanja wa Tanganyika Packers ambapo pia wakazi hao walipata nafasi ya kupima afya zao bure kabisa kwa kufanyiwa vipimo vya ugonjwa wa kisukari chini ya ST LAURENT DIABETES CENTRE E-fm walipoandika goli la kwanza kupitia mshambuliaji...

Like
621
0
Monday, 16 November 2015
MAREKANI YAMSHAMBULIA JIHAD JOHN
Global News

WANAJESHI wa Marekani wametekeleza shambulio la Anga lililomlenga mwanamgambo wa Islamic State kutoka Uingereza ajulikanaye  kwa jina la Jihadi John.   John alilengwa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria kufuatia msimamo wake mkali pamoja na kuonekana kwenye video akiwakata shingo mateka wa kutoka mataifa ya Magharibi. Afisa wa habari wa Pentagon-Peter Cook amesema kuwa wanaamini matokeo ya operesheni ya leo usiku italeta manufaa makubwa kulingana na malengo yao.  ...

Like
191
0
Friday, 13 November 2015
WAPIGANAJI WA KIKURDI WAUTWAA MJI WA SINJAR
Global News

WAPIGANAJI wa Kikurdi wamefanikiwa kuingia mji wa Sinjar kaskazini mwa Iraq, siku moja baada yao kuanza kwa operesheni ya kuutwaa kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State. Wakati hayo yakijiri, jeshi la Iraq limesema limeanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Ramadi magharibi mwa nchi hiyo ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji wa IS. Hata hivyo hatua ya Kuukomboa mji wa Sinjar kutaziba mawasiliano kati ya ngome mbili za IS Raqqa na Mosul....

Like
207
0
Friday, 13 November 2015
MAMA NA BABA LISHE TANZANIA KUANZISHA UMOJA
Local News

JUMUIYA ya Mama na Baba lishe Tanzania inatarajia kuunda umoja wao wenye malengo ya kutoa suluhisho la changamoto zinazowazunguka kwa kuanzisha Shirikisho la Saccos ili kutoa elimu mbalimbali za mkopo na ujasiliamali.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama lishe na Baba lishe Tanzania Ramadhan Mhonzu amesema kuwa malengo na madhumuni ya jumuiya hiyo ni kuunganisha Wadau mbalimbali ili kutoa nafasi za kulinda haki za ajira zao.   Kwa upande wake Katibu...

Like
348
0
Friday, 13 November 2015
ANNE MAKINDA ATANGAZA KUTOWANIA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE NA KUACHANA NA SIASA
Local News

WAKATI viongozi mbalimbali wakijitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekuwa Spika wa Bunge hilo Anne Makinda amesema hatogombea nafasi hiyo na kwamba ameachana na masuala ya kisiasa kwa kuwa amejishughulisha na masuala hayo kwa kipindi cha miaka 40.   Makinda ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wake wa kuwania nafasi hiyo ambayo tayari ameshaipitia.   Akizungumzia namna alivyoweza kuliongoza bunge kwa kipindi alichokuwa...

Like
255
0
Friday, 13 November 2015
POLISI ULAYA WASHIKILIA WATU 17
Global News

POLISI katika nchi sita za Ulaya wamewakamata watu 17, kwa tuhuma za kupanga mashambulizi. Watu hao wengi wao wakiwa ni Wakurd wa Iraq, wanachama wa kundi la Wapiganaji wa Kiislamu wanadaiwa kupanga mashambulizi nchini Norway na Mashariki ya Kati. Hata hivyo Polisi wamesema kundi hilo lilikuwa likijiandaa kufanya mashambulizi ili kumuokoa kiongozi wake, mwenye msimamo mkali, Mullah Krekar anayeshikiliwa nchini Norway....

Like
197
0
Friday, 13 November 2015