Slider

MAMA WAJAWAZITO WAMETAKIWA KUFUATA VIDOKEZO VYA HATARI WAKATI WA UJAUZITO
Local News

IMEELEZWA kuwa vifo vya mama wajawazito vinavyotokea wakati wa kujifungua vinachangiwa na wao kutozingatia vidokezo vya hatari wakati wa ujauzito. Hayo yamesemwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya Dakta GRORIA MBWILLE wakati akizungumza na Efm. Dokta Mbwille Amesema kuwa vifo vingi vimekuwa vikichangiwa na mama wajamzito kutofanya maandalizi mapema kabla ya...

Like
406
0
Thursday, 12 November 2015
MYANMAR: KIONGOZI WA UPINZANI ATOA WITO KUFANYIKA MAZUNGUMZO YA KITAIFA
Global News

KIONGOZI wa upinzani nchini Myanmar Aung Suu Kyi, leo ametoa  wito  wa kuwepo kwa  mazungumzo  ya  kitaifa  ya upatanishi  kati ya rais  wa  Myanmar  na  mkuu  wa  jeshi  la nchi  hiyo  lenye  nguvu  kubwa  kisiasa  baada ya chama chake kuonekana  kupata  ushindi  wa  kishindo katika Uchaguzi mkuu. Chama  cha  National League for  Demcracy-NLD-kimeonekana kupata madaraka  baada  ya  kupata asilimia  90  ya  viti vilivyotangazwa  hadi  sasa sawa na viti 163 kati  ya  viti 182 vilivyotangazwa  hadi sasa....

Like
201
0
Wednesday, 11 November 2015
AFRIKA KUSINI: POLISI WANANE WAFUNGWA JELA
Global News

MAAFISA wanane wa polisi waliopatikana na hatia ya kumfanyia ukatili dereva wa teksi kutoka Msumbiji mwaka 2013 wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja. Maafisa hao walinaswa kwenye kanda ya video wakimburuza dereva wa gari ndogo (teksi) kutoka Msumbuji aliyetambuliwa kwa jina la Macia mwenye umri wa miaka 27 mtaa wa Macia mashariki mwa Johannesburg. Awali kabla ya kutokea kwa tukio hilo Macia alikuwa amesimamishwa na maafisa tisa wa polisi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama...

Like
222
0
Wednesday, 11 November 2015
SERIKALI YAOMBWA KUWACHUKULIA HATUA KALI BAADHI WATUMISHI WA IDARA YA ARDHI
Local News

WAKAZI wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali baadhi ya watumishi wa Idara ya Ardhi kwenye halmashauri ya mji wa Babati kwani wamehusika kusababisha migogoro ya ardhi wilayani humo.   Wakazi hao pia wameeleza kuwa, migogoro mingi ya Ardhi kwenye wilaya hiyo imesababishwa na baadhi ya watumishi wasiokuwa na maadili na wanaojali maslahi yao binafsi badala ya kujali maslahi ya wananchi.   Kwa upande wakes mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela amesema atahakikisha anasimamia vyema...

Like
186
0
Wednesday, 11 November 2015
BAN KI MOON ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA MAGUFULI
Local News

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dokta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano.   Katika salamu zake katibu Mkuu huyo amesema kuwa Uchaguzi wa mwaka huu ni uthibitisho wa wazi na dhamira ya muda mrefu ya Watanzania kwa demokrasia, Amani na utulivu.   Mbali na hayo Ban Ki Moon amesema anaamini kuwa, chini ya uongozi wa Rais...

Like
220
0
Wednesday, 11 November 2015
MPANGO WA CHANJO YA HOMA YA UTI WA MGONGO WAFANIKIWA AFRIKA
Global News

WATAALAMU wa Afya wamesema kuwa mpango wa chanjo kwa umma dhidi ya homa ya uti wa mgongo barani Afrika umepata mafanikio makubwa. Zaidi ya watu milioni mbili walipata kinga dhidi ya maradhi hayo katika nchi 16 barani Afrika, ikiwemo Gambia na Ethiopia. Shirika la Afya Duniani limesema katika kipindi cha mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa wanne wa Uti wa mgongo barani Afrika ingawa awali iliweka rekodi ya kuwa na maelfu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kila...

Like
267
0
Wednesday, 11 November 2015
DONALD TRUMP ASHTUMIWA VIKALI KWA KUPANGA KUTIMUA WAHAMIAJI
Global News

DONALD TRUMP, mmoja wa wanaowania nafasi ya Urais kupitia chama cha Republican katika Uchaguzi mkuu nchini Marekani, ameshutumiwa vikali kutokana na mpango wake wa kuwafukuza wahamiaji milioni 11 kutoka nchini humo. Kwenye mdahalo wa moja kwa moja kupitia runinga, wagombea wengine wawili wanaoshindana naye, John Kasich na Jeb Bush, waliukosoa vikali mpango huo wakisema hauwezi kutekelezeka na ni kitendo cha ubaguzi. Hali hiyo imesababisha watu waliohudhuria mdahalo huo kumzomea Trump, wakati alipojaribu kujitetea kuhusu huo mpango...

Like
185
0
Wednesday, 11 November 2015
WANAWAKE WALIOCHAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU
Local News

MTANDAO wa Jinsia Tanzania-TGNP-pamoja na wanaharakati wa ngazi ya jamii wamewataka wanawake waliochaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kuwajibika kikamilifu kwa kuitumikia jamii kwani ndiyo iliyowapa ridhaa. Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam jana na mkurugenzi wa-TGNP- Bi. Lilian Liundi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi kuanzia hatua ya awali hadi mwisho lengo ikiwa ni kuangalia ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi. LIUNDI amebainisha kuwa kulingana na...

Like
251
0
Wednesday, 11 November 2015
WAFANYAKAZI MUHIMBILI WAMETAKIWA KUWAHI NA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Local News

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ameanza kazi rasmi na kuwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwahi kazini kwa wakati na kufanya kazi kwa bidii.   Profesa Mseru ametoa kauli hiyo jana Jijini Dar es salaam baada ya kukutana na menejimenti ya hospitali hiyo ambayo inajumuisha Wakurugenzi 14.   Profesa Mseru ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo baada ya dokta Hussein Kidanto kuhamishiwa wizara ya...

Like
268
0
Wednesday, 11 November 2015
CHALLENGE 2015: CECAFA YATANGAZA MAKUNDI
Slider

shirikisho la soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limetangaza Makundi matatu ya timu zitakazocheza michuano ya Challenge itakayoanza November 21 na kumalizika December 6.  KUNDI A Ethiopia Tanzania Zambia Somalia KUNDI B Burundi Djibouti Kenya Uganda  KUNDI C Rwanda Sudan Sudan Kusini Zanzibar...

Like
328
0
Wednesday, 11 November 2015
MAREKANI NA ISRAEL ZAKUBALIANA KUWEKA KANDO MVUTANO
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekubaliana kuweka kando mvutano uliosababishwa na kutiwa saini makubaliano ya mradi wa nyuklia wa Iran na kuweka nguvu za pamoja kutetea maslahi ya nchi zao mbili katika eneo la mashariki ya kati.   Wakifanya mkutano wa pamoja kwa mara ya kwanza baada ya kupita miezi 13 katika Ikulu ya Marekani rais Obama amesema wazi kuwa usalama wa Israel ndio suala muhimu.   Rais Obama na waziri mkuu wa...

Like
236
0
Tuesday, 10 November 2015