Slider

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA WIZARA YA FEDHA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza kwa kutembea kwa miguu kutoka Ikulu hadi katika Wizara ya Fedha.   Akiwa Wizarani hapo, Rais Magufuli amekagua utendaji kazi wa wafanyakazi wa  ofisi hizo.   Rais amefanya ziara hiyo muda  mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju. Hata hivyo ziara hiyo ya ghafla ya rais ilikuta baadhi ya maofisa wakiwa nje ya ofisi...

Like
295
0
Friday, 06 November 2015
FA YATUPILIA MBALI RUFAA YA MOURINHO
Slider

Fa imetupilia mbali rufaa ya meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho aliyoikata kupinga faini ya pound 50,000 na kufungiwa mchezo mmoja na shirikisho hilo la soka. Mreno huyo alipigwa faini hiyo kufuatia kauli yake aliyoitoa baada ya timu yake kutandikwa Southampton kwa kudai kuwa waamuzi wa mchezo huo waliogopa kutoa penati kwa klabu...

Like
252
0
Friday, 06 November 2015
MAPIGANO YAONGEZEKA BUJUMBURA
Global News

WATU zaidi wameendelea kutoroka katika  mji wa Bujumbura nchini Burundi baada ya kuongezeka kwa mapigano. Jumatano, watu wanne waliuawa katika mitaa miwili ya mji huo mkuu na  Maafisa wa serikali wanasema watu hao waliuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi kati ya makundi ya watu wenye silaha na maafisa wa polisi usiku. Mauaji yamekuwa yakitokea nchini Burundi tangu Aprili baada ya kuanza kwa maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa...

Like
295
0
Friday, 06 November 2015
AFRIKA YA KUSINI YAPEWA SIKU 60 KUIONDOLEA VIKWAZO MAREKANI
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama ameipa Afrika ya Kusini siku 60 kuondoa vikwazo katika bidhaa za kilimo kutoka Marekani la sivyo ataiondolea msamaha wa kodi wa bidhaa. Mpango huo utaathiri karibu robo ya billion ya dollar ya bidhaa za Afrika kusini zinazosafirishwa nchini Marekani. Afrika Kusini ilipiga marufuku kuagiza mazao ya kuku mwezi Decemba kutokana na kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa mafua ya ndege na kwa miaka kadhaa imekuwa ikitoa adhabu ya kodi kwa baadhi ya bidhaa za kuku...

Like
282
0
Friday, 06 November 2015
HOFU YA KIPINDUPINDU YATANDA MBEYA
Local News

WAKAZI wa jiji la Mbeya wameingiwa na hofu ya kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na mlundikano wa taka katika maeneo yao.   Wakazi hao wameingiwa na hofu hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho mvua inanyeesha na takataka bado zimeendelea kuwepo katika ghuba la kuhifadhia taka kwa muda mrefu.   Akiongelea malalamiko hayo ya wananchi Afisa Afya wa jiji la Mbeya Daktari JOHNSON NDARO amesema wameshindwa kuondoa taka katika makazi ya watu kutokana na ubovu wa magari pamoja na ukosefu...

Like
422
0
Friday, 06 November 2015
GEORGE MASAJU AAPISHWA KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta John Pombe Magufuli, asubuhi ya leo amemwapisha Bwana George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali –AG, herehe zilizo fanyika  Ikulu jijini Dar es saalam.   Mwanasheria Mkuu Masaju ambaye kwa mara ya mwisho aliteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua nafasi hiyo  iliyobaki wazi baada ya aliyekuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema  kujiuzulu.   Tayari Rais Dokta Magufuli ameshaitisha Vikao vya Bunge Novemba 17 na anatarajiwa kumtangaza...

Like
224
0
Friday, 06 November 2015
WANAFUNZI WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA MKUTANO WA CHINA NA TAIWAN
Global News

MAELFU ya wakazi na wanafunzi wameandamana leo nje ya jengo la Bunge la Taiwan, kutokana na kughadhibishwa na mkutano wa kihistoria ulipangwa kufanywa na viongozi wa Taiwan na China.   Rais wa Taiwan  Ma Ying-jeou anatarajiwa kukutana na rais wa China  Xi Jinping  Jumamosi mjini Singapore.   Mashirika ya habari ya umma yameripoti kwamba, mkutano huo utakuwa wa kwanza kwa viongozi wa China na Taiwan kukutana katika kipindi cha miongo...

Like
282
0
Wednesday, 04 November 2015
NDEGE YA MIZIGO YAANGUKA SUDANI KUSINI
Global News

NDEGE ya  mizigo imeanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege nchini Sudan Kusini na kusababisha vifo vya watu takriban  41 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pamoja na waliokuwa maeneo iliko tokea ajali hiyo.   Msemaji wa ofisi ya rais Ateny Wek Ateny amesema muhudumu mmoja na mtoto wamenusurika katika ajali hiyo.   Mwandishi wa shirika la habari wa AP aliyekuwa karibu na eneo la tukio amesema alishuhudia mabaki ya ndege hiyo yalionekana yametawanyika upande wa mashariki...

Like
286
0
Wednesday, 04 November 2015
SERIKALI YA WANAFUNZI UDSM YASIKITISHWA NA UTARATIBU WA UTOAJI MIKOPO
Local News

SERIKALI ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM imesema kuwa imesikitishwa na utaratibu wa kutoa mikopo uliofanywa na Bodi ya mikopo kufuatia asilimia 90 ya Wanafunzi kukosa mikopo ambapo jumla ya Wanafunzi 600 kati ya Wanafunzi zaidi ya elfu 7000 wanaodahiriwa katika chuo hicho ndio waliobahatika kupata mikopo hiyo.   Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Waziri wa Mikopo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Shitindi Venance amesema kuwa wameshangazwa na idadi ya...

Like
412
0
Wednesday, 04 November 2015
RAIS KIKWETE AMEITANGAZA SIKU YA KESHO KUWA NI MAPUMZIKO
Local News

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko. Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015...

Like
322
0
Wednesday, 04 November 2015
MSF YATAKA UCHUNGUZI HURU DHIDI YA MASHAMBULIZI YA NDEGE ZA MAREKANI
Global News

SHIRIKA la madaktari wasio na mipaka-MSF, limerudia kutoa ombi la kufanyika uchunguzi huru, mwezi mmoja baada ya hospitali yake nchini Afghanistan kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani.   Shirika hilo lenye makao yake mjini Paris, jana limefanya mkutano wake mjini New York na kutumia dakika moja kukaa kimya kuwakumbuka watu 30 waliouawa katika shambulizi hilo la anga, lililofanyika kwenye hospitali ya watu walioathirika na vita mjini Kunduz.   Mkurugenzi Mtendaji wa MSF Marekani, Jason Cone, amesema wamekuwa wakifanya kazi...

Like
176
0
Wednesday, 04 November 2015