Slider

HALI YA USALAMA NI TETE HAITI
Global News

HALI katika mji mkuu wa Haiti ni tete baada ya wafuasi wa mgombea mmoja wa kiti cha urais kuleta vurugu kwa kuwasha moto magurudumu ya magari na kuweka vizuzi barabarani. Vurugu hizo zimejiri baada ya mgombea wanaomuunga mkono Moise Jean-Charles, kudai kuwa kura zake zimeteketezwa moto na zingine kufichwa. Hatha hivyo wanaishtumu tume ya uchaguzi nchini humo kwa kukiuka kanuni na utendaji wa uchaguzi huru na wa...

Like
259
0
Friday, 30 October 2015
PAUL RYAN ATEULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE MAREKANI
Global News

MWANASIASA wa chama cha Republican nchini Marekani Paul Ryan ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani. Ryan, anayetoka jimbo la Wisconsin, hakutaka kuwania mwanzoni lakini mwisho alijitosa kwenye kinyang’anyiro na kuungwa mkono na wengi wa wabunge wa Republican katika Bunge la Congress kumrithi John Boehner aliyetoka Ohio. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa mgombea mwenza wa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican Mitt Romney mwaka...

Like
189
0
Friday, 30 October 2015
SERIKALI YAANDAA UTARATIBU KUWEKA MFUMO MPYA WA MAKAZI MISHANO
Local News

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali inaandaa utaratibu wa namna ya kuweka mfumo mpya wa makazi kwenye eneo la Mishamo, wilayani Mpanda ili wakazi hao waondokane na hali ya kuishi kama wakimbizi.   Waziri Pinda ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa eneo hilo waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mpira Mishamo uliokuwa na lengo la kutoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia uraia waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972.  ...

Like
221
0
Friday, 30 October 2015
NEC YAKABIDHI CHETI CHA USHINDI KWA MAGUFULI
Local News

KUFUATIA Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-kumtangaza mgombea wa chama cha mapinduzi-CCM-dokta John Pombe Magufuli kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga wamempongeza kwa kupata ushindi huo. Dokta Magufuli amekabidhiwa cheti cha ushindi leo Jijini Dar es salaam kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC. Hafla ya kukabidhiwa cheti imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano...

Like
185
0
Friday, 30 October 2015
NEC YAMTANGAZA RASMI DOKTA JOHN POMBE MAGUFULI KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Local News

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NCHINI-NEC-IMEMTANGAZA RASMI DOKTA JOHN POMBE MAGUFULI KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIYEKUWA AKIWANIA NAFASI HIYO KUPITIA CHAMA CHA...

Like
225
0
Thursday, 29 October 2015
WANADIPLOMASIA KUKUTANA VIENNA LEO KUIJADILI SYRIA
Global News

WANADIPLOMASIA wa ngazi za juu duniani wanakutana mjini Vienna leo kujaribu kusaka ufumbuzi wa pamoja wa namna ya kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria. Wanadiplomasia hao kutoka Urusi, Marekani, Saud Arabia na Uturuki wanakutana kwa duru ya pili ya mazungumzo kuhusu Syria, baada ya ile ya wiki iliyopita kabla ya kuitishwa mkutano utakaowajumuisha wanadiplomasia wa eneo hilo. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran Javad Zarif atajiunga na wenzake kutoka Uingereza, Misri, Ufaransa, Ujerumani na Umoja...

Like
291
0
Thursday, 29 October 2015
WANAOWANIA TIKETI REPUBLICAN WAJIBIZANA VIKALI
Global News

WANAOWANIA nafasi ya kuwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican jana wamejibizana vikali kwenye mdahalo wa tatu ulioandaliwa katika jimbo la Colorado. Donald Trump na Ben Carson, ambao hawana uzoefu mkubwa kisiasa lakini ndio wanaoongoza kinyang’anyiro hicho, wameshambuliwa kwenye mdahalo huku Gavana wa Ohio John Kasich akiukashifu mpango wake “wa ndoto kuhusu ushuru”. Hata hivyo Pendekezo lake kuhusu ushuru, lilishutumiwa vikali na Kasich, ambaye pia alishutumu vikali mpango wa Trump wa kuwaondoa wahamiaji milioni 11...

Like
177
0
Thursday, 29 October 2015
SERIKALI YASHAURIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA WAKATI WAKUSUBIRI MATOKEO YA UCHAGUZI
Local News

SERIKALI imeshauriwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi katika wizara mbalimbali hususani kipindi hiki wakati wananchi wanasubiri viongozi wa awamu ya tano kuingia madarakani.   Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Dodoma na mmiliki wa shamba la mazao mbalimbali mkoani Manyara Papuu Dharampal wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.   Dharampal ameiomba serikali pia kuangalia suala la wakulima wadogo na wa kati kwa kuwapatia masoko ili waweze kunufaika na kilimo na kwaajili ya maendeleo...

Like
223
0
Thursday, 29 October 2015
WIZARA YA UCHUKUZI YAZINDUA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI HODHI YA RASILIMALI NA MIUNDOMBINU
Local News

WIZARA ya uchukuzi leo imezindua bodi ya wakurugenzi wa kampuni hodhi ya rasilimali na miundombinu ya reli nchini  RAHCO. Akizindua bodi hiyo kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo mheshimiwa Samuel Sitta, katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi dokta Shabani Mwinjaka amesema lengo  kubwa la kuundwa kwa bodi hiyo ni kuhakikisha wajumbe wanasimamia taratibu, kanuni na sheria za uchukuzi. Aidha dokta Mwinjaka amebainisha kuwa uundwaji wa bodi hiyo umeezingatia mahitaji ya Taifa ya sasa ambapo njia ya reli imekuwa ikihitajika...

Like
280
0
Thursday, 29 October 2015
AU YALAANI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU SUDANI KUSINI
Global News

MUUNGANO wa Afrika umelilaumu Jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita. Uchunguzi wa AU umebaini kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda Rais. Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu...

Like
228
0
Thursday, 29 October 2015
NEPAL YAPATA RAIS WA KWANZA MWANAMKE
Global News

BUNGE la nchini Nepal limemchagua mtetezi wa haki za wanawake Bidhya Devi Bhandari kuwa rais wa kwanza mwanamke, katika hatua ambayo imetajwa kuwa ya kihistoria. Mwanamke huyo wa miaka 54 kwa sasa ndiye Naibu mwenyekiti wa chama tawala cha kikomunisti ambaye awali alikuwa waziri wa ulinzi mwaka 2009 na 2011. Bhandari atachukua nafasi ya Ram Baran Yadav, aliyekuwa rais wa kwanza wa Taifa hilo kuchaguliwa na watu mwaka 2008 baada ya Nepal kufuta utawala wa...

Like
355
0
Thursday, 29 October 2015