CHAD YATANGAZA HALI YA HATARI

CHAD YATANGAZA HALI YA HATARI

Like
331
0
Tuesday, 10 November 2015
Global News

CHAD imetangaza hali ya hatari eneo la Ziwa Chad baada ya kuongezeka kwa mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram kutoka Nigeria.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya watu wawili kuuawa katika shambulio la kujitoa mhanga linalodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo hao.

Boko Haram wanashukiwa kuhusika katika mauaji ya watu wawili katika kijiji kimoja nchini Chad Jumapili iliyopita na wakimbizi watatu kutoka Nigeria kaskazini mwa Cameroon jana.

Comments are closed.