CHAMA CHA ACT KIMETANGAZA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA

CHAMA CHA ACT KIMETANGAZA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA

Like
383
0
Tuesday, 03 February 2015
Local News

BAADA ya hivi karibuni kujitokeza kwa  migogoro baina ya viongozi wa Chama cha Alliance for Change –ACT,  Chama hicho kimeamua kufanya marekebisho ya katiba ya chama  ili kukinusuru na migogoro ya namna hiyo.

Akizungumza na EFM Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama SAMSONI MWIGAMBA amesema kuwa Marekebisho hayo yatasaidia kusuruhisha  migogoro inayojitokeza kwa baadhi ya viongozi wanaotumiwa kukivuruga  chama.

Amebainisha kuwa katiba mpya imerekebisha mapungufu ya katiba ya awali ambayo ilikuwa haina kamati ya nidhamu na maadili katika chama pia ilikuwa haitambui kuwepo kwa mwenyekiti mkuu wa chama.

 

Comments are closed.