CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KIMETOA TAMKO LA KUTOTAMBUA MKUTANO ULIOFANYWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO

CHAMA CHA WAFUGAJI NCHINI KIMETOA TAMKO LA KUTOTAMBUA MKUTANO ULIOFANYWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO

Like
604
0
Wednesday, 04 February 2015
Local News

CHAMA CHA WAFUGAJI Tanzania-CCWT kimetoa tamko la kutotambua mkutano uliofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa GEORGE SIMON kuanzisha chama kingine cha wafugaji kwa madai ya kutofuata sheria na Katiba zilizounda chama hicho.

Tamko hilo limekuja kufuatia Mkutano Mkuu wa Wanachama wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma January 24 na 25 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa- CCWT ALLY LUMIYE amesema kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho alikumbwa na tuhuma za kuchapisha Kadi na Vitabu feki vya Stakabadhi hali inayosababisha Kamati Tendaji imsimamishe kujihusisha na shughuli zote za utendaji ndani na nje ya chama hadi hapo itakapoamriwa vinginevyo.

 

Comments are closed.