CHAMA cha maalbino nchini kimesifu uamuzi wa serikali wa kuwapiga marufuku waganga wa kienyeji wanaosababisha ongezeko la mauaji ya watu hao wenye ulemavu wa Ngozi nchini- Albino.
Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Waziri wa mambo ya ndani, nchini , Mathias Chikawe amesema kwamba msako wa kitaifa utaanza hivi karibuni kuwakamata waganga hao na kuwafikisha mahakamani ikiwa wataendelea na kazi zao.
Watu wenye ulemavu wa ngozi, wanakabiliwa na tisho kubwa juu ya maisha yao, kwani wamekuwa wakilengwa kwa sehemeu zao za mwili na waganga pamoja na wapiga ramli wanaoamini kwamba viungo hivyo huleta bahati ya kupata mali.