CHAMA CHA WANANCHI CUF CHASITISHA MAANDAMANO

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHASITISHA MAANDAMANO

Like
274
0
Friday, 13 February 2015
Local News

CHAMA cha Wananchi CUF, kimetangaza kusitisha Maandamano yaliyokuwa yafanyike leo ambayo yaliandaliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha wananchi- Cuf- JUVICUF.

JUVICUF iliandaa maandamano hayo kwa lengo la kufikisha ujumbe wao kwa waziri wa mambo ya ndani juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la Polisi pamoja na kuitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza siku za uandikishaji wa daftari la kudumu la wapika kura kutoka siku saba za sasa na hadi siku 14.

Hapo jana Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wa Kanda maalumu ya Dar es salaam, Suleiman Kova aliwataka JUVICUF kutii Sheria na kuacha kuandamana kwani kwa kufanya hivyo jeshi la polisi litafanya kazi kwa mujibu wa Sheria.

 

Comments are closed.