CHELSEA NA LIVERPOOL ZATINGA ROBO FAINALI ENGLAND

CHELSEA NA LIVERPOOL ZATINGA ROBO FAINALI ENGLAND

Like
399
0
Wednesday, 29 October 2014
Slider

Chelsea na Liverpool zatinga katika hatua ya robo fainali ya kombe la ligi nchini England kwa ushindi wa magoli 2-1 kila mmoja.

Chelsea bila ya mshambuliaji wao tegemezi msimu huu, Diego Costa ilibidi wamgeukie Didier Drogba aliyefunga goli la kwanza katika mchezo huo likiwa ni goli lake la tatu katika michezo mitatu iliyopita ndani ya uzi wa The Blues.

Mnamo dakika ya 77 klabu ya Shrewsbury ilifanikiwa kusawazishakabla ya beki wa klabu hiyo Grandison kujifunga katika daika ya 81.

Wakati huohuo klabu ya Liverpool imepata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Swansea huku Mario Balotteli akionyersha kiwango kizuri baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Rickie Lambert ambapo The Kops walikuwa nyuma kwa goli moja.

Beki ya Swansea ilionekana iko imara mpaka mnamo dakika ya 94 beki wa kimataifa wa Croatia, Dejan Lovren alipounganisha krosi kwa kichwa na kupeleka furaha kwa vijana wa Brendan Rodgers.

Comments are closed.