RAIS wa China, Xi Jinping na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe wamefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu wote washike madaraka.
Mkutano wao unaonekana kama hatua ya ufanisi ya juhudi za kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya nchi hizo kutokana na madai ya Japan kuthibiti visiwa katika bahari ya kaskazini mwa China.
Baada ya dakika thelathini za mazungumzo Bwana Abe aliondoka na kusema kuwa hiyo ndiyo hatua ya kwanza ya kuboresha mahusiano.
Mkutano huo ulifanyika Beijing wakati viongozi kutoka katika maeneo ya Asia wamekutana katika kongomano la kibiashara la APEC.