CHINA YAIDHINISHA HATUA KADHAA KUNUSURU SOKO

CHINA YAIDHINISHA HATUA KADHAA KUNUSURU SOKO

Like
199
0
Tuesday, 07 July 2015
Global News

SERIKALI ya China imeidhinisha hatua kadhaa mwishoni mwa juma kulishinikiza soko ambalo limepoteza takriban asilimia 30 ya thamani yake katika wiki tatu zilizopita kurudi katika hali yake.

Wawekezaji wengi wana wasiwasi na kwamba robo ya kampuni zilizoorodheshwa kuomba kusitisha kuuza hisa zao zinasababisha uwezo wa serikali kukopa unazidi kuwa katika hatari.

Taarifa zaidi zinaonesha kuwa hali hiyo ni kama hatua ya kuzilinda kampuni hizo dhidi ya hasara zaidi ambapo kwa kipindi cha mwaka uliopita serikali ilifurahia uwekezaji katika soko la hisa kwa kupata faida zaidi ya mara mbili.

 

Comments are closed.