CUF KUSIMAMA MAHAKAMANI KUPINGA MATOKEO MAJIMBO 6

CUF KUSIMAMA MAHAKAMANI KUPINGA MATOKEO MAJIMBO 6

Like
218
0
Tuesday, 03 November 2015
Local News

KUFUATIA dosari mbalimbali zilizojitokeza katika baadhi ya Majimbo ya uchaguzi wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu Chama cha Wananchi-CUF-kinatarajia kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge katika majimbo sita Nchini.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Afisa haki za binadamu na Sheria Taifa wa chama hicho Muhamedi Mluwa amesema kumekuwa na dosari nyingi katika uchaguzi mkuu jambo ambalo limesababisha chama hicho kushindwa.

 

Mluwa ameyataja baadhi ya majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Pangani, Mtwara vijijini, Newala, Lindi mjini na Tabora njini amba[po pia amebainisha kuwa baadhi ya dosari hizo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa vya Uchaguzi.

Comments are closed.