DAVID KAFULILA AOMBA UFAFANUZI JUU YA SWALA LA ESCROW BUNGENI LEO

DAVID KAFULILA AOMBA UFAFANUZI JUU YA SWALA LA ESCROW BUNGENI LEO

Like
548
0
Tuesday, 04 November 2014
Local News

 

MKUTANO wa 16 na 17 wa kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo mjini Dodoma ambapo kumekuwa na kipindi cha maswali na majibu mara baada ya kusomwa kwa mara ya pili Miswaada ya Sheria ya Serikali pamoja na Mswaada Binafsi wa bajeti wa mwaka 2014.

 

Katika majadiliano hayo yaliyoambatana na kipindi cha maswali na majibu ya masuala mbalimbali ya maendeleo ndipo muda ulipofika kwa baadhi ya wabunge kuomba miongozo ya masuala muhimu kutolewa ufafanuzi ambapo Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini DAVID KAFULILA kuomba ufafanuzi juu ya suala la ESCROW

 

Hata hivyo Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu WILLIUM LUKUVI amemuomba Mbunge huyo na Wabunge wengine kuwa na subira kwani uchunguzi wa –CAG unatarajiwa kukamilika hivi karibuni japo hakutaja tarehe rasmi.

 

 

Comments are closed.