DAVID MOYES ATEULIWA KUWA MENEJA WA REAL SOCIEDAD

DAVID MOYES ATEULIWA KUWA MENEJA WA REAL SOCIEDAD

Like
428
0
Tuesday, 11 November 2014
Slider

Aliyekuwa kocha wa kikosi cha Manchester United, David Moyes ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa klabu ya Real Sociedad inayokipiga ndani ya ligi kuu nchini Hispania (LA LIGA).

Moyes amesaini mkataba wa miezi kumi na nane akichukua nafasi ya kocha aliyefungashiwa virago Jacob Arraste ikiwa ni miezi nane tu toka alipotimuliwa ndani ya Manchester United.

Klabu ya Real Sociedad inashika nafasi ya kumi na tano katika msimamo wa La Liga ikiwa imejikusanyia jumla ya alama tisa tu sawa na vilabu vinne vilivyo chini ya klabu hiyo na alama tatu tu juu ya klabu inayoshika mkia katika ligi hiyo.

Moyes anatarajia kuanza kazi rasmi tarehe ishirini na mbili mwezi huu katika mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna huku michezo minne inayofuatia ni dshidi ya Elche, Oviedo (kombe la mfalme), Villareal na Athletic Club Bilbao.

Real-Sociedad-v-Olympique-Lyonnais-UEFA-Champions-League-Play-offs-Second-Leg

Comments are closed.