DK SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA

DK SLAA ATANGAZA RASMI KUACHANA NA SIASA

Like
265
0
Tuesday, 01 September 2015
Local News

ALIYEKUWA katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo –CHADEMA- Dokta WILBROAD SLAA ametangaza rasmi kuachana na siasa isipokuwa ataendelea kuwa mtumishi wa kawaida kwa watanzania.

 

Dokta Slaa ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya azma yake ya kujihusisha na masuala ya kisiasa nchini kwa kipindi cha maisha yake.

 

Aidha katika mkutano wake na waandishi wa habari amesema kuwa hata kama hatojihusisha na siasa na chama chochote cha siasa atahakikisha anasimamia msimamo wake wa kuwatetea watanzania katika matumizi ya rasilimali zilizopo nchini.

 

Comments are closed.