DONALD TRUMP AKOSOLEWA VIKALI

DONALD TRUMP AKOSOLEWA VIKALI

Like
252
0
Wednesday, 16 December 2015
Global News

WAGOMBEA wa Republican wanaowania nafasi ya urais nchini Marekani wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea kwa mashambulio ya California na Paris.

Mgawanyiko mkubwa umetokea kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea haki za kiraia.

Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani, huku Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, akimwita Trump kuwa ni mgombea anayependa vurugu.

 

Comments are closed.