DONDO ZA MBIO ZA MAGARI ZA FORMULA 1

DONDO ZA MBIO ZA MAGARI ZA FORMULA 1

Like
1092
0
Thursday, 06 November 2014
Slider

Dereva wa kimataifa kutoka nchini Brazil, Felipe Nasr ameteuliwa kuitumikia timu ya Sauber yenye maskani yake huko nchini Uswisi katika michuano ya langalanga msimu wa 2015.

Felipe aliyekuwa ni dereva wa akiba wa timu ya Williams atajiunga na timu inayoshika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi huku wakishindwa kukusanya alama yoyote.

Uteuzi huo unamaanisha kuwa madereva wawili wa sasa Adrian Sutil na Esteban Gutierez watakuwa huru kujiunga na timu nyengine ndani ya klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Felipe mwenye umri wa miaka 22 atasaidiwa na Marcus Ericsson, 24 aliyejiunga na timu hiyo akitokea Claterham iliyofilisika mwezi uliopita

Comments are closed.