Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Australia Matthew Hayden ameshangazwa na maamuzi ya timu ya taifa ya England ya kumuacha nahodha wa zamani wa timu hiyo, Kevin Pietersen.
Matthew amesema kitendo cha England kumuacha mmoja kati ya wachezaji hodari kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya nchi ya England kinaonyesha wazi hawapo teyari kwenda kushindana na timu kama India na Australia.
England wametangaza majina ya wachezaji 15 watakaoshiriki michuano ya kombe la dunia huku ikimteua Eoin Morgan kuwa nahodha wa timu hiyo mbele ya mchezaji mkongwe Alastair Cook.
Timu hiyo ipo katika kundi linalojumuisha timu za Australia, New Zealand, Scotland, Sri Lanka, Bangladesh, Afghanistan.