DZEKO ATUA ROMA KWA MKOPO

DZEKO ATUA ROMA KWA MKOPO

Like
228
0
Thursday, 13 August 2015
Slider

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Edin Dzeko amejiunga na klabu ya Roma ya Italia kwa mkopo wa muda mrefu huku uhamisho wake ukitazamwa kama uhamisho wa kudumu, ilitangaza klabu ya Manchester City ya England.

Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Bosnia alijiunga na Man City akitokea Wolfsburg mwaka 2011akiwa na rekodi ya kushinda magoli 72 katika michezo yake 189.

Katika msimu uliopita mchezaji huyu hakuhusishwa sana na michezo ya klabu ya Man City hali iliyopelekea apate ushindi wa magoli sita tu.

Huku msimu wake wa kwanza alioshiriki kikamilifu aliweka rekodi ya magoli 19 katika michezo 42

Dzeko,mwenye miaka 29, anaondoka kwenye klabu ya Man City huku klabu hiyo ikitwaa ubingwa mara mbili ikiwa ni Premier League pamoja na FA Cup.

Comments are closed.