EL NINO KUATHIRI MAMILIONI YA WATU 2016

EL NINO KUATHIRI MAMILIONI YA WATU 2016

Like
230
0
Wednesday, 30 December 2015
Global News

MASHIRIKA ya misaada yamesema kuwa hali ya hewa ya El Nino ambayo imekuwa ndiyo kali zaidi katika historia itazidisha hatari ya njaa na maradhi kwa mamilioni ya watu duniani 2016.

 

Hali hii ya hewa inatarajiwa kusababisha ukame baadhi ya maeneo na mafuriko kwingine, ambapo baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika sana yako Afrika, huku uhaba wa chakula ukitarajiwa kufikia kilele mwezi Februari.

 

Hali ya hewa ya El Nino, hutokana na kuongezeka kwa joto na huathiri hali ya hewa maeneo mengi. Mwaka huu hali hii imezidi na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika historia.

Comments are closed.