ENGLAND: BLATTER NI KIKWAZO KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2026

ENGLAND: BLATTER NI KIKWAZO KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2026

Like
262
0
Wednesday, 25 March 2015
Slider

Baada ya kukosa nafasi ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2018 kwa kuambulia kura mbili na kubwagwa na urusi katika nafasi hiyo sasa England inafikiria kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026.

Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini England Greg Dyke amesema jaribio lao litategemea kama rais wa FiFa Sepp Blatter hataendelea kusalia madarakani lakini pia kuteuliwa kwa mwingereza David Gill katika kamati ya kuu ya uongozi ya Fifa inaweza kuongeza ushawishi.

Hata hivyo Greg amesema England itachukua hatua hiyo iwapo tu sera zitakuwa wazi lakini haitaomba kuwa mwenyeji wa fainali wakati Blatter akiwa bado yupo madarakani.

UK2 UKKK

Comments are closed.