BUNGE la Jamhuri ya muungano wa Tanzania leo linaanza mjadala kuhusu sakata la wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta –ESCROW- kutokana na zoezi la kugawa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali-CAG- na ya Takukuru kwa wabunge wote kukamilika.
Taarifa zinaeleza kuwa mjadala huo unaanza kwa wabunge mara baada ya kamati ya –PAC- ikiongozwa na mbunge wa kigoma kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi bungeni.
Mbali na hayo suala la muingiliano wa madaraka kati ya bunge na mahakama limeonesha kuwa kikwazo katika mjadala huo ingawa spika wa bunge mheshimiwa ANNE MAKINDA, amesisitiza kuendelea kwa mjadala huo bungeni kama kawaida.