EU YAJADILI KUKATA MSAADA BURUNDI

EU YAJADILI KUKATA MSAADA BURUNDI

Like
199
0
Friday, 24 July 2015
Global News

MUUNGANO wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kukata msaada wake nchini Burundi na inakisiwa kuwa fedha kutoka muungano huo unafikia zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya Burundi ya kila mwaka.

 

Mkuu wa masuala ya mambo ya nje wa Muungano wa EU Federica Mogherini, ameelezea wasiwasi wake juu ya ghasia zilizototokea nchini humo kabla ya kufanyika  kwa uchaguzi wa rais, na ametilia shaka iwapo serikali itakayoundwa baada ya uchagzi huo itakuwa wakilishi ya taifa nzima.

Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu umetajwa kwenda kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha.

 

Comments are closed.