FERGUSON ATAJA TOP 4 KATIKA KIPINDI CHAKE

FERGUSON ATAJA TOP 4 KATIKA KIPINDI CHAKE

Like
245
0
Tuesday, 22 September 2015
Slider

Aliyewahi kuwa meneja wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amesema ni wachezaji wanne tu ambao wanaingia kwenye orodha ya wachezaji bora duniani aliowahi kufanya nao kazi katika kipindi cha miaka 26 ya utumishi katika fani yake.
Mwalimu huyu ambae anarekodi ya kutwaa taji la klabu bingwa mara mbili na mataji 13 ya ligi kuu ya Uingereza mara 13 akiwa na kikosi cha Man U alitaja wachzaji hao wakati wa mahojiano yake na kituo cha BBC.
Ferguson alianza kumtaja kiungo Paul Scholes, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs kama wachezaji bora kuwahi kutokea katika kipindi chake.

Ferguson, 73, alimzungumzia Cantona, aliesajiliwa kutoka kutoka klabu ya Leeds November 1992 akiongeza kuwa alipomnunua mchezaji huyu alifanikiwa kutwaa taji la ligi kuu katika msimu huo huku akimzungumzia pia Ronaldo kama genius

Comments are closed.