GHOROFA LATEKETEA KWA MOTO DAR

GHOROFA LATEKETEA KWA MOTO DAR

Like
287
0
Tuesday, 10 February 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kutii sheria na kukaa pembeni ya Barabara pindi wasikiapo ving’ola vya hatari ili kurahisisha shughuli za uokoaji wa maisha ya watu na mali.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa kikosi cha zima moto kanda maalum ya Dar es salaam Esward Ikonko alipokuwa Katika ajali ya moto iliyotokea leo eneo la Kariakoo na mnazi mmoja katika mtaa Jamhuri jijini Dar es salaam ambapo amesema moja ya changamoto inayosababisha magari ya zima moto kuchelewa katika eneo latukio ni msongamano wa watu.

Moto huo ambao baadae ulidhibitiwa kwa ushirikiano wa jehi la zimamoto na jeshi la polisi nchini umetokea katika Jengo la Consolidated Company Limited ghorofa ya pili na kuteketeza ghorofa hiyo pamoja na mali zote zilizokuwepo ndani, japo moto huo haukusababisha maafa kwa binadamu.

Photo0104

Comments are closed.