WATUMAIJI WA TEKNOLOJIA YA INTERNET WATAKIWA KUITUMIA HUDUMA HIYO KUONGEZA MAARIFA

WATUMAIJI WA TEKNOLOJIA YA INTERNET WATAKIWA KUITUMIA HUDUMA HIYO KUONGEZA MAARIFA

Like
192
0
Tuesday, 10 February 2015
Local News

WATUMIAJI wa teknolojia ya interneti nchini wametakiwa kutumia teknolojia hiyo kutafuta taarifa mbalimbali za maarifa na zenye  mwelekeo wa kuleta maendeleo badala ya kutumia teknolojia hiyo kutafuta taarifa zisizo na faida na zenye mwelekeo wa kupotosha kizazi cha sasa kimaadili.

Wito huu umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia, katika siku ya matumizi ya interneti duniani iliyoadhimishwa leo duniani kote ambako amesema kuwa Vodacom kama kampuni ya mawasiliano siku zote itakuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi  bora na sahihi ya mtandao wa interneti.

Mbali na biashara amesema kuwa interneti imejaa maarifa ya kielimu ya taaluma mbalimbali ambazo zinafanya dunia kuwa kijiji kimoja hivyo matumizi mazuri ya interneti yanaweza kumfanya mtu popote alipo kupata taarifa na maarifa ya taaluma anayohitaji au taarifa anazotaka kujua kwa haraka.

Comments are closed.