GODON BROWN AMEUTAKA ULIMWENGU KULAANI VITENDO VYA BOKO HARAM KUTUMIA WATOTO

GODON BROWN AMEUTAKA ULIMWENGU KULAANI VITENDO VYA BOKO HARAM KUTUMIA WATOTO

Like
284
0
Friday, 16 January 2015
Global News

MJUMBE maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Elimu GORDON BROWN, ameutaka Ulimwengu kulaani kutumiwa kwa Wasichana wadogo na kundi la waasi wa Boko Haram nchini Nigeria, kama washambuliaji wa kujitoa mhanga kwa kujilipua.

BROWN ambaye ni Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza, amekiita kitendo hicho kuwa  Unyama mpya, wa waasi hao.

Matamshi yake yamekuja baada ya ripoti kwamba Boko Haram imewatumia wasichana watatu kufanya mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwishoni mwa Wiki iliyopita.

Comments are closed.