Hakuna kiwango cha pombe kilicho salama kwa afya yako

Hakuna kiwango cha pombe kilicho salama kwa afya yako

Like
766
0
Thursday, 03 January 2019
Slider

Ni habari mbaya kwa wale wanaofurahia kile wanachofikiri ni kikombe kimoja cha divai kwa siku.

Utafiti mpya wa kimataifa ulimwenguni uliochapishwa katika jarida la Lancet umethibitisha utafiti uliopita ambao umeonyesha kwamba hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe.

Watafiti wanakubali kwamba unywaji wa kiwango cha kadri unaweza kukulinda dhidi ya ugonjwa ya moyo lakini waligundua kwamba hatari ya saratani na magonjwa huzidi faida yoyote ya pombe mwilini.

Mwandishi wa utafiti alisema matokeo yake yalikuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya mambo mengi yalioangaziwa.

Utafiti wa magonjwa ulimwenguni uliangazia kiwango cha matumizi ya pombe na madhara yake ya afya katika nchi 195, ikiwemo Uingereza kati ya 1990 na 2016.

Uchambuzi wa data miongoni mwa watu wenye kati ya umri wa miaka 15 hadi 95, watafiti walitofautisha kati ya watu wasiotumia pombe kabisa na wale ambao hutumia kikombe kimoja cha pombe kwa siku.

Waligundua kwamba kati ya watu 100,000 wasiokunywa pombe, 914 watakuwa na tatizo la afya linalohusiana na pombe ama kupata madhara.

Lakini watu wanne zaidi wataathiriwa iwapo watakunywa kikombe kimoja cha pombe kwa siku.

Kwa watu ambao waliokunywa vikombe viwili vya pombe kwa siku, watu 63 zaidi walipata madhara katika kipindi cha ndani ya mwaka mmoja na kwa wale waliokunywa vikombe vitano vya pombe kila siku kulikuwa na watu 338 zaidi waliopata madhara ya kiafya.

Mmoja wa waandishi wa utafiti huo, Profesa Sonia Saxena, mtafiti katika chuo cha Imperial mjini, alisema: “Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku unaongeza hatari ndogo lakini ikilinganishwa na idadi kuu ya raia wa London inawakilisha idadi kubwa na kwamba wengi wao hawatumii kikombe kimoja kwa siku.

Mwandishi anayeongoza utafiti huo Dk Max Griswold, katika Taasisi ya Matibabu na Tathmini ya Afya (IHME), Chuo Kikuu cha Washington, alisema: “Uchunguzi uliopita umeonyesha kinga ya pombe kwa hali fulani, lakini tumegundua kwamba hatari za pamoja za kiafya za pombe huongezeka kwa kiasi kwa kutumia kiwango chochote cha pombe.

“Ushirika wa juu kati ya matumizi ya pombe na hatari ya saratani, majeruhi, na magonjwa ya kuambukiza hupunguza madhara ya kinga ya ugonjwa wa moyo katika utafiti wetu.

“Ingawa hatari za afya zinazohusiana na pombe huanza kuwa ndogo kwa kunywa kikombe kimoja kwa siku, na huongezeka kwa haraka kadri ya watu wanapoendelea kunywa zaidi.”

Mnamo mwaka wa 2016, serikali ilipunguza viwango vya pombe ilivyopendekeza kwa wanaume na wanawake kutozidi 14 kwa wiki – sawa na chupa sita za pombe ya wastani au glasi saba zamvinyo

Wakati huohuo, Profesa Dame Sally Davies, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza, alisema kuwa kiasi chochote cha pombe kinaweza kuongeza hatari ya saratani.

Prof Saxena alisema utafiti huo ulikuwa ni utafiti muhimu zaidi uliofanywa juu ya somo hilo.

Alielezea: “Utafiti huu umepiga hatua zaidi kuliko mwengine kwa kuzingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mauzo ya pombe, taarifa za kujitegemea juu ya kiasi cha kunywa pombe, kujizuia, data ya utalii, viwango vya biashara haramu na pombe zinazotengezwa nyumbani.”

Utafiti huo unaonyesha kwamba wanawake wa Uingereza hunywa vinywaji wastani vya chupa tatu za pombe kwa siku na wameorodheshwa katika nafasi ya nane katika ulimwengu wa watu wanaobugia viwango vya juu vya pombe.

Wanaume wa Uingereza kwa kulinganisha, wako katika nafasi ya 62 kati ya nchi 195 zilizofanyiwa utafiti, ingawa pia hunywa wastani wa chupa tatu za pombe kwa siku.

Hii ni kwa sababu viwango vya unywaji pombe vilikuwa vya juu zaidi kwa ujumla kati ya wanaume, na wanaume wa Kiromania hunywa vinywaji zaidi ya nane kila siku.

Kinywaji kilielezewa kuwa na gramu 10 za pombe, ambayo inafanana na glasi ndogo ya divai, chupa ya bia, au whisky.

Kote duniani, mtu mmoja kati ya watu watatu wanakunywa pombe na inahusishwa na vifo vyote kwa wale wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49

Prof Saxena alisema: “Wengi wetu nchini Uingereza hunywa zaidi ya mipaka salama, na kama utafiti huu unaonyesha hakuna viwango salama.

Mapendekezo yanahitaji kuwafikia watu wengi zaidi na serikali inapaswa kufikiria upya sera yake.

Iwapo unataka kunywa, jifunze mwenyewe kuhusu hatari, na kuchagua hatari unayoijua”

cc;- bbcswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *