HALI SI SHWARI MAREKANI

HALI SI SHWARI MAREKANI

Like
320
0
Tuesday, 25 November 2014
Global News

GHASIA zimezuka nchini Marekani, baada ya Wanasheria kuamua kutomfungulia Mashtaka Polisi wa Kizungu aliyeua Kijana Mweusi.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Vitu mbalimbali vimechomwa moto, baada ya jopo la Wanasheria nchini humo kuamua kutomfungulia Mashtaka polisi DAREN WILSON, ambaye amemuua kwa kumpiga risasi kijana Mweusi MICHAEL BROWN.

Tukio hilo lilitokea katika mji wa Ferguson mwezi Agusti mwaka huu.

Kwa upande wake Rais wa Marekani BARACK OBAMA ametaka kuwepo kwa amani, licha ya kueleweka kwamba baadhi ya raia wa nchi hiyo watakuwa wamesikitishwa na kuingiwa na hasira na uamuzi huo wa Marekani.

 

Comments are closed.