HISPANIA YASUBIRI MAJIBU YA UCHAGUZI

HISPANIA YASUBIRI MAJIBU YA UCHAGUZI

Like
253
0
Monday, 21 December 2015
Global News

CHAMA cha kihafidhina cha nchini Hispania kinachoongozwa na Waziri Mkuu Mariano Rajoy kimeshinda katika uchaguzi mkuu lakini kimeshindwa kupata wingi wa kura za kutosha za kukiwezesha kuunda serikali ijayo.

Rajoy amesema atajaribu kuunda serikali mpya iliyo thabiti baada ya chama chake cha Popular-PP-kushinda kwa asilimia 28.71 na hivyo kujinyakulia viti 123 vya Ubunge.

Chama cha Kisosholisti kiliibuka mshindi wa nafasi ya pili katika uchaguzi huo kwa kupata viti tisini huku vyama viwili vipya vya Podemos na cha mrengo wa kati cha Ciudadonos vikiwa katika nafasi ya tatu na nne.

Comments are closed.