MAHAKAMA mjini Kampala leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ambapo wanaume 13 wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na al-Shabaab mwaka 2010.
Watu zaidi ya 70 walifariki kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa wakati watu wakitazama fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2010.
Kesi hiyo imechukua miaka sita.