ICC YATAKA  JOSEPH KONY AKAMATWE NA KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA HIYO

ICC YATAKA JOSEPH KONY AKAMATWE NA KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA HIYO

Like
285
0
Thursday, 22 January 2015
Global News

MWENDESHA  Mkuu wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC Fatou Bensouda ametaka kuwepo kwa juhudi mpya za kumkamata kiongozi wa kundi la waasi la Uganda la Lord’s Resistance Army LRA Joseph Kony baada ya kamanda wa ngazi ya juu wa kundi hilo Dominic Ongwen kufikishwa katika mahakama hiyo jana  kujibu mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Bensouda amesema waathiriwa wa madhila yaliyofanywa na kundi la LRA linaloongozwa na Kony wamesubiri kwa muda mrefu kwa haki kutendeka.

Ongwen amefikishwa katika kizuizi cha mahakama hiyo jana ambako atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kufikishwa mbele ya majaji, wiki mbili baada ya kujisalimisha kwa wanajeshi wa Marekani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

 

Comments are closed.