IS YATHIBITISHA KUUA MATEKA WAWILI

IS YATHIBITISHA KUUA MATEKA WAWILI

Like
230
0
Thursday, 19 November 2015
Global News

WAPIGANAJI wa Islamic State (IS) wamethibitisha kuwaua mateka wawili, ambao ni raia wa Norway na raia wa China.

Waziri mkuu wa Norway Erna Solberg amesema hakuna sababu zozote za kutilia shaka tangazo la wapiganaji hao na kutaja kitendo chao kuwa ni “unyama”.

Naye Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hong Lei amesema kwamba tangu raia huyo nchi yake akamatwe, Taifa hilo limefanya jitihada za kumuokoa bila mafanikio.

Comments are closed.