TAASISI YA MISA YAZINDUA RIPOTI MAALUM KUANGALIA HALI YA VYOMBO VYA HABARI

TAASISI YA MISA YAZINDUA RIPOTI MAALUM KUANGALIA HALI YA VYOMBO VYA HABARI

Like
309
0
Thursday, 19 November 2015
Local News

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-MISA-kwa kushirikiana na Taasisi binafsi ya Friedrich Ebert Stiftung jana imezindua rasmi ripoti maalum ya kuangalia hali ya Vyombo vya habari ilivyo nchini kwa kuangazia masuala muhumu ya kiutafiti kwa nia ya kupima mwenendo na hali ya vyombo vya habari.

 

Ripoti hiyo imelenga kutoa uchambuzi wa hali halisi ya namna Vyombo vya Habari nchini vinavyofanya kazi zake kwa uhuru na kwa kuzingatia sera, sheria na kanuni za uendeshaji wa vyombo hivyo.

 

Akizungumzia ripoti hiyo Mwenyekiti wa Taasisi ya-MISA-Simon Berege amesema kuwa ripoti ya tafiti hiyo inaonesha kuwa madaraja ya mishahara na mazingira ya kazi ya Waandishi wa habari nchini sio nzuri  kutokana na hali halisi kuwa Waandishi wengi hawajaajiriwa suala ambalo ni changamoto katika utendaji wao wa kazi.

 

Comments are closed.