RAIS MAGUFULI AMTEUA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

RAIS MAGUFULI AMTEUA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

Like
288
0
Thursday, 19 November 2015
Local News

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea jina la Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya Tano ambaye ni mheshimiwa KASSIM MAJALIWA Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi-CCM.

Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais Mamlaka ya kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge.

Kabla ya kutajwa kwa jina lake katika nafasi ya Uwaziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa alikuwa Naibu waziri aliyeshughulikia masuala ya Elimu kupitia-TAMISEMI.

Comments are closed.