WAZIRI MKUU wa Israel BENJAMIN NETANYAHU amekataa kuwa na mazungumzo juu ya kujiondoa kwa Israel mjini Jerusalem na katika Ukingo wa Magharibi kwa kipindi kisichozidi miaka miwili.
Bwana NETANYAHU ametoa kauli hiyo kabla ya kukutana na Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani JOHN KERRY hii leo.
Israel imeteka maeneo ya Jerusalem, Gaza na Ukingo wa Magharibi wakati wa Vita vya Siku Sita mwaka wa 1967 na kujiondoa mjini Gaza mwaka wa 2005.
Bwana NETANYAHU amebainisha kuwa kujiondoa katika maneno hayo kwa sasa kutasababisha Wanamgambo walio na Itikadi kali kuingia katika vitongoji vya Tel Aviv na hatimaye mjini Jerusalem.