ISRAEL YATOA WITO KWA MATAIFA YENYE NGUVU KUIADHIBU IRAN

ISRAEL YATOA WITO KWA MATAIFA YENYE NGUVU KUIADHIBU IRAN

Like
340
0
Monday, 14 March 2016
Global News

ISRAEL imetoa wito kwa mataifa yenye nguvu duniani kuiadhibu Iran kwa jaribio lake la hivi karibuni la kurusha makombora ya masafa marefu.

 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inapeleka dai hilo kwa Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani-mataifa ambayo yamesaini mpango wa kuiondoshea Iran vikwazo kwa makubalino ya taifa hilo kuachana na mpango wake wa nyuklia.

 

Netanyahu amesema Iran imekwenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu majaribio ya makombora, na mataifa hayo yenye nguvu yaliahidi kuidhibiti Iran katika ukiukwaji huo.

 

Comments are closed.