ITAMBOLEO: WANANCHI WAMKALIA KOONI MTENDAJI WA KIJIJI KUFUATIA UBADHILIFU WA FEDHA

ITAMBOLEO: WANANCHI WAMKALIA KOONI MTENDAJI WA KIJIJI KUFUATIA UBADHILIFU WA FEDHA

Like
368
0
Friday, 08 January 2016
Local News

WANANCHI wa Kijiji cha Itamboleo Kata ya Chimala Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamemtaka Mkugunzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,  kumchukulia hatua za nidhamu Mtendaji wa Kijiji Julius Mwagala kwa ubadhilifu wa fedha za kijiji.

 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Itamboleo SAMWEL KAGANGA amesema kuwa Mwagala amekula shilingi laki 9 zilizochangwa na wananchi mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo ya Kijiji.

 

Hata hivyo inaelezwa kuwa, mtendaji huyo hajafika kazini tangu mwezi March mwaka jana  ambapo kazi zake zimekuwa zikifanywa na Afisa Kilimo wa Kijiji JESCA MAHENGE

Comments are closed.