SERIKALI imeombwa kuisaidia jamii ya watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kuhakikisha wanapata elimu kwani hadi sasa ni asilimia 10 pekee ndiyo wanaopata elimu.
Akizungumza na kituo hiki Katibu wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) amesema kuwa Tanzania ina zaidi ya watu million sita wenye ulemavu mbalimbali hivyo ni vema wakasaidiwa kupata elimu ili kuondokana na tatizo la kuitegemea jamii na serikali kuwasaidia kuyaendesha maisha yao.