JAMII YA WAFUGAJI IMETAKIWA KUTOKOMEZA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

JAMII YA WAFUGAJI IMETAKIWA KUTOKOMEZA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Like
240
0
Monday, 16 November 2015
Local News

JAMII ya wafugaji imetakiwa kutumia juhudi katika kubadili mitazamo ya watu juu ya matumizi ya mila na desturi ili kusaidia kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kuleta maendeleo kwa Taifa.

 

Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari vya kijamii Bi. Rose Haji Mwalimu wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la viongozi wa mila wa kabila la wamasai na wanawake Mashuhuri lenye lengo la kushawishi uondoaji wa mila potofu zinazorudisha nyuma maendeleo.

 

Bi. Rose amewataka washiriki wa warsha kusimama na kutumia vyema elimu waliyoipata kuishawishi jamii kubadilika na kuachana na mila za ukekeketaji na ndoa za utotoni.

Comments are closed.