JANUARY MAKAMBA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMATI YA FEDHA YA BUNGE LA FINLAND

JANUARY MAKAMBA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMATI YA FEDHA YA BUNGE LA FINLAND

Like
345
0
Tuesday, 12 April 2016
Local News

WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa kamati ya fedha ya Bunge la Finland.

 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, wabunge hao wameipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazozifanya za kulinda na kuhifadhi mazingira.

 

Awali akiwakaribisha wabunge hao, Waziri Makamba amesema Tanzania inajivunia uhusiano bora uliopo baina yake na Finland na kuwashukuru wabunge hao kwa kufanya ziara yao nchini.

Comments are closed.